Juan Guaidó

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Juan Guaidó

Juan Gerardo Guaidó Márquez (alizaliwa 28 Julai 1983) ni mhandisi na mwanasiasa wa Venezuela ambaye pia ni Rais wa Bunge la Venezuela toka tarehe 5 Januari 2019. Ni mwanachama wa chama cha Popular Will.

Tarehe 23 Januari 2019, wakati wa mgogoro wa urais wa Venezuela, Guaidó alijitangaza kuwa rais wa muda wa Venezuela huku nchi hiyo ikiwa tayari na rais ambaye ni Nicolás Maduro. Hadi Februari 2019, madai yake ya kuwa rais kutokana na tafsiri mojawapo ya Katiba ya Venezuela, yametambuliwa na zaidi ya nchi 50.

Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Juan Guaidó kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.