Joyce Lazaro Ndalichako
Mheshimiwa Prof Joyce Ndalichako Mb | |
Waziri wa elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi
| |
Aliingia ofisini 2015 | |
Rais | John Magufuli |
---|---|
aliyemfuata | Shukuru Kawambwa |
Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA)
| |
Muda wa Utawala 2005 – 2014 | |
mtangulizi | Dr Charles Msonde |
Mbunge
| |
Muda wa Utawala 2015 – 2020 | |
Appointed by | John Magufuli |
Constituency | Hana jimbo (Mbunge wa viti maalam) |
tarehe ya kuzaliwa | 21 Mei 1964 Musoma, Mara |
utaifa | Mtanzania |
chama | CCM (1982–sasa) |
mhitimu wa | University of Dar Es Salaam (B.Sc. with Education), University of Alberta (PhD) |
dini | Mkristo |
Joyce Lazaro Ndalichako (alizaliwa Musoma, 21 Mei 1964) ni mwanasiasa Mtanzania na mwanachama wa Chama cha kisiasa cha CCM. Aliteuliwa[1] na Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli kuwa mbunge na pia Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi kwa miaka 2015 – 2020 nchini Tanzania[2] akiendelea hata katika awamu ya sita chini ya Samia Suluhu Hassan.
Elimu yake
[hariri | hariri chanzo]Joyce Ndalichako alipata shahada yake ya kwanza katika Ualimu (kwa Kiingereza: Bachelor of Science with Education, majoring in Mathematics), akijikita katika Hisabati, katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam nchini Tanzania mnamo mwaka 1987 hadi 1991. Alipata shahada yake ya Uzamivu katika Saikolojia ya Elimu (Kiingereza: PhD in Educational Pyschology, major in Educational Statistics & Measurement and Evaluation), akijikita katika Takwimu za Kielimu na Vipimo vya Kielimu pamoja na Tathmini ya Elimu, katika Chuo Kikuu cha Alberta nchini Kanada. [3]
Kazi yake
[hariri | hariri chanzo]- Mnamo mwaka 2000 hadi 2005, Joyce Ndalichako alikuwa ni mhadhiri mkuu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akifundisha masuala ya Vipimo vya Kielimu na Tathmini ya Elimu, mbinu za Utafiti na Takwimu za Kielimu, huku akisimamia kazi (Kiingereza: dissertation) za wanafunzi wake.[4][3]
- Kuanzia mwaka 2014 hadi leo, Joyce Ndalichako ni profesa msaidizi na mkuu msaidizi kwa upande wa Utafiti katika Chuo Kikuu cha Agha Khan, Taasisi ya Maendeleo ya Elimu, Afrika Mashariki.[3][4]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-12-25. Iliwekwa mnamo 2017-05-13.
- ↑ Tovuti ya Bunge la Tanzania, iliangaliwa Mei 2017
- ↑ 3.0 3.1 3.2 "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-07-25. Iliwekwa mnamo 2020-07-25.
- ↑ 4.0 4.1 "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-08-19. Iliwekwa mnamo 2020-07-25.