Nenda kwa yaliyomo

Josip Mrzljak

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Josip Mrzljak (alizaliwa Vukovar, 19 Januari 1944) alikuwa askofu wa Jimbo Katoliki la Varaždin kutoka 2007 hadi 2019.

Baba yake, Vladimir, alipotea mnamo 1945 na inadhaniwa aliuawa na Wanamgambo wa Kikomunisti wa Yugoslavia.

Mrzljak alipewa daraja ya upadre mnamo 1969 na Kardinali Franjo Kuharić.

Papa Yohane Paulo II alimteua kuwa askofu msaidizi wa Zagreb tarehe 29 Desemba 1998, akapewa daraja ya uaskofu tarehe 6 Februari 1999.[1]

Papa Benedikto XVI alimteua kuwa Askofu wa Varaždin mnamo 20 Machi 2007.

Papa Fransisko alikubali ombi lake la kustaafu tarehe 1 Agosti 2019.

  1. (in it) Rinunce e Nomine, 01.08.2019 (Press release). Holy See Press Office. 1 August 2019. http://press.vatican.va/content/salastampa/it/bollettino/pubblico/2019/08/01/0614/01266.html. Retrieved 1 August 2019.
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.