Joshua Bassett
Joshua Taylor Bassett (alizaliwa 22 Desemba 2000)[1] ni muigizaji na mwimbaji wa Marekani. Alianza kazi yake kama muigizaji wa utotoni, akitokea katika msimu wa tatu wa tamthilia ya vichekesho ya familia ya Disney Channel iitwayo Stuck in the Middle (2018)[2] kama Aidan Peters. Bassett alipata umaarufu mkubwa kwa uhusika wake mkuu kama mwanafunzi wa shule ya upili Ricky Bowen katika mfululizo wa vipindi vya mtandaoni vya Disney+ vya High School Musical: The Musical: The Series (2019–2023), na kwa nyimbo zilizosindikiza mfululizo huo, ambazo zilimfanya ateuliwa kuwania Tuzo mbili za Children's and Family Emmy, akishinda mnamo mwaka 2023.[3]
Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Bassett alizaliwa na kulelewa huko Oceanside, California, kwa wazazi wake Taylor na Laura. Ana dada watano na alisomea nyumbani (home-schooled).[4][5]
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Kuanzia mwaka 2017 hadi 2018, Bassett alitokea kwenye nafasi ndogo za vipindi vya hapa na pale (episodic roles) katika tamthilia za televisheni za: Lethal Weapon, Game Shakers, na Dirty John. Uhusika wake mkubwa wa kwanza ulikuwa mwanzoni mwa mwaka 2018 kama Aidan Peters katika msimu wa tatu na wa mwisho wa tamthilia ya vichekesho ya Disney Channel iitwayo Stuck in the Middle.[6]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://tvovermind.com/joshua-bassett/
- ↑ https://lumiere-a.akamaihd.net/v1/documents/disney_bio_-_joshua_bassett_38f21730.pdf
- ↑ https://deadline.com/2020/01/joshua-bassett-high-school-musical-the-musical-the-series-hollywood-agency-uta-1202847048/
- ↑ https://www.sandiegouniontribune.com/2019/12/26/from-regional-theater-to-breakout-disney-star-oceanside-native-joshua-bassett-reflects-on-his-rise/
- ↑ https://highschool.latimes.com/arts-and-entertainment/high-school-musical-the-musical-the-series-winks-to-the-past-with-a-modern-take/
- ↑ https://deadline.com/2018/10/high-school-musical-the-musical-joshua-bassett-star-ricky-disney-series-1202484645/
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Joshua Bassett kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |