Nenda kwa yaliyomo

Josette Abondio

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Josette Desclercs Abondio au Josette Abondio (alizaliwa 1949) ni mwalimu, mwandishi na mtunzi wa tamthilia kutoka Kodivaa.

Maisha ya awali na elimu

[hariri | hariri chanzo]

Josette Desclercs Abondio alizaliwa mwaka 1949[1] nchini Kodivaa, na lugha yake ya kwanza ni Kifaransa. Alianza kupenda vitabu akiwa mtoto na akawa msomaji hodari. Abondio alifanya kazi kama mwalimu wa shule ya sekondari[2] pamoja na mkufunzi wa mawasiliano ya kiufundi.

Kazi ya uandishi

[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 1993 aliandika riwaya *Kouassi Koko...ma mère*, inayozungumzia maisha ya mwanamke anayekuwa mke wa pili (concubine) baada ya kifo cha mtu aliyekuwa akimsaidia.[onesha uthibitisho]

Kazi yake nyingine muhimu ni kitabu cha watoto kilichochapishwa 1999, *Le rêve de Kimi*.[3]

Abondio alikuwa rais wa tatu wa Chama cha Waandishi wa Kodivaa (AECI) kuanzia 1998 hadi 2000. Mwaka 2010 alishirikiana na Flore Hazoumé katika jarida *Scrib Spiritualité*.[1]

Mwaka 2013 alikuwa akiendesha duka la vitabu Abidjan.[2]

Maisha binafsi

[hariri | hariri chanzo]

Abondio anapenda sana sanaa ya karate na ni mwenye cheti cha mkanda mweusi (black belt).[onesha uthibitisho]

  • *Kouassi Koko...ma mère* (1993)[4]
  • *Le rêve de Kimi* (1999)[3]
  • *Le jardin d'Adalou* (2012)
  • *La dernière ruse de compère araignée* (2013)
  • *Le royaume du cœur* (2013)[2]
  • *Tant qu’elle aime: Nouvelles* (2015), mkusanyiko wa hadithi fupi[5]
  1. 1 2 [(https://library.osu.edu/literary-map-of-africa/authors/abondio-josette) Josette Abondio], OSU.edu, Retrieved 8 April 2016
  2. 1 2 3 [(http://aflit.arts.uwa.edu.au/AbondioJosetteEng.html)[dead link] Josette Abondio], University of Western Australia, Retrieved 7 April 2016
  3. 1 2 [(http://www.africultures.com/php/?nav=personne&no=12688) Josette Abondio], AfriCultures.com, Retrieved 8 April 2016
  4. Kouassi Koko...ma mère. Edilis. 1993. ISBN 2909238075. OCLC 33194315.
  5. Tant qu'elle aime: Nouvelles. Les Classiques Ivoiriens. 2015. ISBN 9782372230148. OCLC 956633971.
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Josette Abondio kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Kosa la Lua katika package.lua kwenye mstari wa 80: module 'Module:Authority control/auxiliary' not found.