Joseph Diescho
Joseph Diescho (alizaliwa Andara, Mkoa wa Kavango,[1] 10 Aprili 1955 [2]) ni mwandishi na mchambuzi wa masula ya kisiasa kutoka Namibia. Mnamo mwaka 1988, aliandika Born of the Sun, riwaya ya kwanza kuandikwa na mwandishi mzawa wa Namibia . [3]
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Diescho alihudhuria chuo kikuu cha Fort Hare nchini Afrika Kusini ambako alisomea sheria na sayansi ya siasa. Wakati wa masomo yake alijihusisha na harakati dhidi ya mfumo wa ubaguzi wa rangi na akafungwa katika magereza ya Peddie na East London. Baadaye alipokuwa akifanya kazi katika kampuni ya mgodi wa almasi alisaidia kuanzisha chama cha wafanyakazi. Mwaka 1984, alipata ufadhili wa masomo wa fulbright katika chuo kikuu cha Columbia jijini New York, ambako alikamilisha shahada yake ya Uzamivu(PHD) katika sayansi ya Siasa mwaka 1992. tasnifu yake iliyobeba kichwa cha "The Role of Education in Politics of Control in Namibia 1948-1988", ilichunguza uhusiano kati ya siasa na elimu nchini Namibia.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Joseph Diescho Archived 11 Juni 2011 at the Wayback Machine Namibia Institute for Democracy
- ↑ Tonchi, Victor L; Lindeke, William A; Grotpeter, John J (2012). Historical Dictionary of Namibia. Historical Dictionaries of Africa, African historical dictionaries (tol. la 2). Scarecrow Press. uk. 87. ISBN 9780810879904.
- ↑ Making a Literature: The Case of Namibia Author(s): Michael Chapman Source: English in Africa, Vol. 22, No. 2 (Oct. 1995), pp. 19–28 Published by: Institute for the Study of English in Africa, Rhodes University
| Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Joseph Diescho kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |