José dos Santos Garcia
Mandhari
José dos Santos Garcia, S.M.P. (16 Aprili 1913 – 11 Desemba 2010) alikuwa askofu wa Kanisa Katoliki kutoka Ureno. Wakati wa kifo chake akiwa na umri wa miaka 97, alikuwa miongoni mwa maaskofu wakongwe zaidi wa Kanisa Katoliki na askofu mkongwe zaidi wa Kireno.
Garcia alizaliwa Aldeia do Souto, Ureno mwaka 1913 na akapadrishwa tarehe 25 Juni 1938 kwa shirika la Missionários da Boa Nova. Mnamo tarehe 5 Aprili 1957, aliteuliwa kuwa askofu wa Port Amelia, Msumbiji, na akapewa daraja la uaskofu tarehe 16 Juni 1957. Alijiuzulu tarehe 15 Januari 1975, muda mfupi kabla ya Msumbiji kupata uhuru kutoka Ureno.[1]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]| Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |