Nenda kwa yaliyomo

José Câmnate na Bissign

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

José Câmnate na Bissign (alizaliwa Mansôa, 28 Mei 1953) ni askofu wa Kanisa Katoliki kutoka Guinea Bisau. Alikuwa askofu wa kwanza mzawa wa Guinea-Bissau, akihudumu kuanzia mwaka 2000 hadi 2020.

Alipadrishwa tarehe 31 Desemba 1982, akiwa na umri wa miaka 29. Baada ya kifo cha Settimio Ferrazzetta, aliteuliwa kuwa askofu wa pili wa Jimbo la Bissau tarehe 15 Oktoba 1999. Alipewa daraja ya uaskofu tarehe 12 Februari 2000.

Askofu Câmnate na Bissign alihusika sana katika mazungumzo kati ya makundi mbalimbali ya kisiasa na kidini nchini Guinea-Bissau. Alikuwa mmoja wa waasisi wa Tume ya Haki na Amani pamoja na Baraza la Mazungumzo ya Kiekumeni, Kidini, na Uendelezaji wa Heshima ya Binadamu.

Papa Fransisko alikubali ombi lake la kustaafu tarehe 11 Julai 2020.[1]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.