Nenda kwa yaliyomo

John Trevenant

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

John Trevenant (pia hujulikana kama Trefnant au Tresnant; katika baadhi ya vyanzo anaitwa Thomas Trevenant; alifariki 29 Machi 1404) alikuwa Askofu wa Hereford.

Aliteuliwa tarehe 5 Mei 1389 na akapewa daraja ya uaskofu tarehe 20 Juni 1389. Trevenant alitoka katika kijiji cha Trefnant, Kaskazini mwa Welisi. Kulingana na R. G. Davies katika Oxford Dictionary of National Biography, Mfalme Richard II wa Uingereza alimweleza Papa kwamba Trevenant alikuwa na uhusiano wa karibu na baadhi ya waheshimiwa waliomuunga mkono, ambao huenda walikuwa Lords Appellant, hasa maearl wa Arundel.[1]

Katika mchakato wa kumwondoa madarakani Richard II, Trevenant alihusika kwa kiwango kikubwa pamoja na Richard Scrope.

  1. Fryde, et al. Handbook of British Chronology p. 251
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.