John Singleton
| Taarifa za jumla | |
|---|---|
| Jinsia | mume |
| Nchi ya uraia | Marekani |
| Jina katika lugha mama | John Singleton |
| Jina la kuzaliwa | John Daniel Singleton |
| Jina halisi | John |
| Jina la familia | Singleton |
| Tarehe ya kuzaliwa | 6 Januari 1968 |
| Mahali alipozaliwa | Los Angeles |
| Tarehe ya kifo | 28 Aprili 2019, 29 Aprili 2019 |
| Mahali alipofariki | Los Angeles |
| Chanzo cha kifo | vifo vya kawaida |
| Sababu ya kifo | cerebral hemorrhage, Shinikizo la juu la damu, kiharusi |
| Sehemu ya kuzikwa | Forest Lawn Memorial Park |
| Mwenzi | Akosua Busia, Abena Busia |
| Mtoto | Justice Singleton, Maasai Singleton |
| Lugha zinazozungumzwa, zilizoandikwa au zilizotiwa sahihi | Kiingereza |
| Muda wa kazi | 1991 |
| End of work period | 2019 |
| Tuzo iliyopokelewa | star on Hollywood Walk of Fame |
| Tovuti | http://www.johnsingletonfilms.com |
| Related category | Category:Films directed by John Singleton, Category:Films with screenplays by John Singleton |
John Daniel Singleton (6 Januari 1968 – 28 Aprili 2019) alikuwa mwongoza filamu, mwandishi wa filamu, na mtayarishaji kutoka Marekani. Alifanya ulimwengu umtambue alipoandika na kuongoza filamu yake ya kwanza ya Boyz n the Hood (1991), ambayo ilimfanya ateuliwe kuwania Tuzo za Akademi kama Mwongozaji Bora wa Filamu. Akiwa na umri wa miaka 24, alikuwa Mmamarekani Mweusi wa kwanza na mtu mdogo zaidi kuwahi kuteuliwa katika kategori hiyo.[1]
Singleton aliendelea kuandika na kuongoza filamu zingine kama vile filamu ya mahaba na tamthilia ya Poetic Justice (1993), tamthilia ya kuelimisha jamii inayohusu maisha ya chuo ya Higher Learning (1995), tamthilia ya kihistoria ya Rosewood (1997), filamu ya jinai ya Shaft (2000), tamthilia ya makuzi ya kijana Baby Boy (2001), pamoja na filamu za mapigano za 2 Fast 2 Furious (2003) na Four Brothers (2005). Kwenye upande wa televisheni, alishirikiana kuunda tamthilia ya jinai ya Snowfall na kuongoza visa vya vipindi kama Empire, Rebel, pamoja na kipindi cha tano cha The People v. O. J. Simpson: American Crime Story. Kupitia kazi hiyo ya mwisho, aliteuliwa kuwania Tuzo za Primetime Emmy.
Akiwa mmoja wa waongozaji waliofanikiwa na kuleta mapinduzi makubwa katika Sinema za Wamarekani Weusi, Singleton na filamu zake ziliwakilisha maisha ya mijini ya Wamarekani Weusi, akimulika mada kama vile ujanadume wa mtu mweusi, mshtuko wa kisaikolojia, ubaguzi wa rangi, na utambulisho. Mara kwa mara Singleton aliwashirikisha wanamuziki wa rap na waimbaji kwenye nafasi kuu za filamu zake, akiwemo Ice Cube, Tupac Shakur, Janet Jackson, Q-Tip, Busta Rhymes, Tyrese Gibson, Snoop Dogg, Ludacris, na André 3000.
Maisha ya awali na elimu
[hariri | hariri chanzo]John Singleton alizaliwa mnamo 6 Januari 1968, huko Los Angeles, akiwa mtoto wa Shelia Ward-Johnson (baadaye Morgan), aliyekuwa afisa mauzo wa kampuni ya dawa, na Danny Singleton, aliyekuwa wakala wa majengo na mshauri wa kifedha.[2] Katika mahojiano ya mwaka 1993 na jarida la DIRT, Singleton alieleza kuhusu maisha yake ya utotoni kwa kusema: "Nilipokuwa nikikua, vitabu vya vibonzo, michezo ya video, na filamu ndivyo vilivyokuwa hifadhi yangu dhidi ya dawa za kulevya na starehe zote [...] Sikukua na Wazungu wengi. Nilikulia katika mtaa wa watu weusi."[3] Alisoma katika Shule ya Sekondari ya Eisenhower, Shule ya Sekondari ya Blair, Chuo cha Pasadena City, na Chuo cha Sanaa za Filamu cha USC.
Singleton alijiunga na chama cha wanafunzi cha Beta Omega cha Kappa Alpha Psi mnamo mwaka 1987, na alitunukiwa shahada yake kutoka Chuo Kikuu cha Southern California (USC) mnamo 1990. Mwanzo alifikiria kusomea sayansi ya kompyuta, lakini baadaye alijiunga na programu ya Uandishi wa Filamu katika chuo cha USC chini ya Margaret Mehring.[4] Programu hiyo ilitengenezwa ili kuwaandaa wanafunzi kuingia moja kwa moja kwenye mfumo wa Hollywood kama waandishi na waongozaji mahiri.
Filmografia
[hariri | hariri chanzo]Filamu
[hariri | hariri chanzo]| Mwaka | Jina la filamu | Mwongozaji | Mwandishi | Mtayarishaji | Mtayarishaji mkuu wa vibao vya filamu |
|---|---|---|---|---|---|
| 1991 | Boyz n the Hood | Ndiyo | Ndiyo | Hapana | Ndiyo |
| 1993 | Poetic Justice | Ndiyo | Ndiyo | Ndiyo | Ndiyo |
| 1995 | Higher Learning | Ndiyo | Ndiyo | Ndiyo | Ndiyo |
| 1997 | Rosewood | Ndiyo | Hapana | Hapana | Ndiyo |
| 2000 | Shaft | Ndiyo | Ndiyo | Ndiyo | Ndiyo |
| 2001 | Baby Boy | Ndiyo | Ndiyo | Ndiyo | Ndiyo |
| 2003 | 2 Fast 2 Furious | Ndiyo | Hapana | Hapana | Ndiyo |
| 2005 | Four Brothers | Ndiyo | Hapana | Hapana | Ndiyo |
| 2011 | Abduction | Ndiyo | Hapana | Hapana | Ndiyo |
|
Mtayarishaji pekee
|
Mtayarishaji Mkuu
|
Nafasi za uigizaji
| Mwaka | Jina la filamu | Wahusika | Maelezo |
|---|---|---|---|
| 1991 | Boyz n the Hood | Tarishi | |
| 1994 | Beverly Hills Cop III | Afisa wa zimamoto | |
| 1995 | Your Studio and You | Yeye mwenyewe | Filamu fupi; Hajaandikwa kwenye majina |
| 2000 | Shaft | Polisi aliyechoka mwenye kikombe cha chai | Hajaandikwa kwenye majina |
| 2001 | Baby Boy | Mtu anayeuza filamu za kukopi | |
| 2003 | Baadasssss! | Detroit J |
Mchango mwingine
| Mwaka | Jina la filamu | Wadhifa |
|---|---|---|
| 2002 | sIDney | Mshauri wa mwongoza filamu (Mentor) |
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "How John Singleton Made History as the Oscars' First Black Best Director Nominee". IndieWire. Aprili 29, 2019. Iliwekwa mnamo 2020-08-03.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "John Singleton Biography (1968–)". Film Reference. Iliwekwa mnamo Oktoba 8, 2010.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Chambers, Veronica (1993). "Singleton". DIRT Magazine. Na. 5. uk. 28.
- ↑ "Margaret Mehring". USC School of Cinematic Arts. Septemba 3, 2008. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Agosti 19, 2010. Iliwekwa mnamo Oktoba 8, 2010.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)