Nenda kwa yaliyomo

John Shalikashvili

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
John Shalikashvili

Picha rasmi, 1993
Amezaliwa (1936-06-27)27 Juni 1936
Warsaw, Jamhuri ya Pili ya Poland
Elimu
  • Chuo Kikuu cha Bradley
  • Chuo Kikuu cha George Washington
Cheo Jenerali
Watoto 2

John Malchase David Shalikashvili (27 Juni 1936 – 23 Julai 2011) alikuwa jenerali wa jeshi la nchi kavu la Marekani aliyeshika wadhifa wa Kamanda mkuu wa majeshi ya muungano Ulaya kuanzia mwaka 1992 hadi 1993 na kuwa mwenyekiti wa wakuu wa vikosi vya pamoja wa 13 kuanzia mwaka 1993 hadi 1997.[1] Alizaliwa mjini Warsaw, Polandi, katika familia ya afisa mkimbizi wa Kigojia (taifa la nchi ya Georgia), Dimitri Shalikashvili, na mke wake Maria Rüdiger-Belyaeva aliyekuwa amepata uraia wa Polandi. Mnamo mwaka 1996, alikuwa mshindi wa kwanza wa tuzo ya uongozi wa wahitimu waliotukuka wa chuo cha vita vya wanamaji.[2]

Shalikashvili alikuwa Mwenyekiti wa kwanza, na hadi kufikia mwaka 2023 ndiye pekee, wa wakuu wa vikosi vya pamoja ambaye hakuzaliwa nchini Marekani. Alitumikia katika kila ngazi ya amri ya vikosi kuanzia ngazi ya kikosi kidogo cha askari (platoon) hadi ngazi ya divisheni.[3] Shalikashvili alifariki kwa kiharusi mnamo mwaka 2011 akiwa na umri wa miaka 75.[4]

  1. ↑ Marble, Andrew (2019). Boy on the Bridge: The Story of John Shalikashvili's American Success. University Press of Kentucky. doi:10.2307/j.ctvn5tz24. ISBN 978-0-8131-7802-8. JSTOR j.ctvn5tz24. S2CID 202496492.
  2. ↑ "USNWC official website". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Novemba 5, 2011.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. ↑ Luttwak (Agosti 22, 1993). "Why Clinton Called Upon Shalikashvili". The Sacramento Bee.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. ↑ Dewan, Shaila (Julai 23, 2011). "Gen. John M. Shalikashvili, Military Chief in 1990s, Dies at 75". The New York Times.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu wakimbizi au masuala ya ukimbizi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu John Shalikashvili kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.