John McEnroe
John McEnroe (Alizaliwa 16 Februari, 1959) ni mchezaji wa zamani wa tenisi nchini Marekani[1]. Alikuwa mchezaji namba 1 duniani katika mechi za mchezaji mmoja (singles) kwa wiki 170 na namba 1 katika mechi za wachezaji wawili (doubles) kwa wiki 269. Ni mmoja wa wachezaji wawili tu katika historia walioshika nafasi ya kwanza katika aina zote mbili za mechi.[2]
McEnroe alizaliwa Wiesbaden, Ujerumani Magharibi, lakini alikulia New York. Alishinda mataji 77 ya wachezaji mmoja na 77 ya mchezaji wawili katika taaluma yake, ikiwemo mataji saba ya Grand Slam katika mechi za wachezaji mmoja (Wimbledon mara tatu na US Open mara nne) na mataji tisa ya wachezaji wawili.[3] Mwaka 1984, aliweka rekodi ya ushindi wa 82 na kushindwa 3 tu, ambayo ndio asilimia bora zaidi katika historia ya tenisi katika msimu mmoja.[3]