John Edward Gray

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 18:00, 9 Machi 2013 na Addbot (majadiliano | michango) (Bot: Migrating 40 interwiki links, now provided by Wikidata on d:q191963 (translate me))
(tofauti) ← Pitio lililotangulia | Toleo la sasa (tofauti) | Pitio linalofuata → (tofauti)
John Edward Gray

John Edward Gray (2 Februari 18007 Machi 1875) alikuwa mtaalamu Mwingereza wa zoolojia wakati wa karne ya 19.

Alizaliwa mtoto wa baba mfarmasia aliyekusanya mimea. Mwenyewe alisoma tiba mjini London na mwaka 1824 aliajiriwa na idara ya zoolojia kwenye Makumbusho ya Kibritania. Akaendelea kuwa mkurugenzi wa idara hii tangu 1840 akaiongoza hadi 1874.

Wakati wake ilikuwa kipindi cha uenezaji wa Milki ya Britania kote duniani na hii ilimsaidia kuongeza sana sampuli za wanyama wa kila aina kutoka pande zote za dunia. Chini ya uongozi wake mkunsanyiko wa kisayansi wa sampuli za wanyama uliendelea kuwa bora duniani.

Kazi hii ilimleta kuainisha mamia ya spishi za wanyama na ndege na kwa hiyo jina lake linakumbukwa katika majina ya spishi alizotangulia kueleza kisayansi.

Alipenda pia stempu za posta alikuwa kati ya watu wa kwanza duniani waliokusanya stempu.

Mdogo wake George Robert Gray alimfuata kaka akaongoza idara ya ndege kwenye makumbusho na kuwa maarufu pia katika uainishaji wa ndege na vipepeo hasa.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu John Edward Gray kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.