John Canemaker
John Cannizzaro Jr. (anajulikana zaidi kama John Canemaker, alizaliwa 1943) ni mchoraji wa vikaragosi huru , mwanahistoria wa uchoraji wa vikaragosi, mwandishi, mwalimu, na mhadhiriwa Marekani.
Mnamo mwaka 1980, alianza kufundisha na kuendeleza programu ya uchoraji wa vikaragosi katika Chuo Kikuu cha New York (NYU), Tisch School of the Arts, taasisi ndogo ya Kanbar Institute of Film and Television Department. Tangu mwaka 1988 amekuwa akiendesha programu hiyo na kwa sasa ni profesa mwenye mkataba wa kudumu. Kuanzia mwaka 2001 hadi mwaka 2002 alikuwa Kaimu Mwenyekiti wa Idara ya Filamu na Televisheni kwa Wanafunzi wa Shahada ya Kwanza katika NYU.
Mnamo mwaka 2006, filamu yake The Moon and the Son: An Imagined Conversation, kazi ya uchoraji wa vikaragosi ya dakika 28 kuhusu uhusiano wa Canemaker na baba yake, ilishinda Tuzo ya Academy kwa filamu bora fupi ya uchoraji wa vikaragosi. Mwaka uliofuata, 2007, kazi hiyo hiyo ilipata Tuzo ya Emmy kwa ubunifu wake wa kimaonyesho na kisanaa.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- John Canemaker's Animated Eye
- John Canemaker Animation Collection at NYU Fales Library
- "My Oscar Experience: An Interview with John Canemaker": Part 1, Part 2
| Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu John Canemaker kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |