Nenda kwa yaliyomo

John Amanam

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

John Amanam (alizaliwa 14 Novemba 1988) ni msanii wa uchongaji sanamu na mtengenezaji wa vifaa bandia vya mwili vinavyofanana kabisa na asili kutoka Nigeria. Anatambulika kama Mwafrika wa kwanza kutengeneza vifaa hivi bandia vinavyofanana sana na mwili halisi. [1][2][3][4]

[5][6][7][8]

Maisha ya awali na elimu

[hariri | hariri chanzo]

John Amanam anatoka Nsit-Atai, Jimbo la Akwa Ibom, lakini alizaliwa na kukulia Calabar, Jimbo la Cross River. Alisoma chuo cha Federal Government , Ikot Ekpene, kisha alisomea Sanaa za Ufundi na Viwanda katika Chuo Kikuu cha Uyo.

Amanam awali alifanya kazi kama msanii wa athari maalumu katika filamu za Nollywood. Alianza kazi yake ya kutengeneza vifaa bandia vinavyofanana kabisa na mwili baada ya ndugu yake kupoteza sehemu ya mkono wake mwaka 2018, na vifaa vilivyopo kuwa vyeupe sana na havikufaa kwa mwili wala tamaduni zao. Prosthetic yake ya kwanza alitengeneza mwaka 2019 na kumkabidhi ndugu yake.

Yeye ni mwanzilishi wa Immortal Cosmetic Art Ltd, Kampuni yake inatengeneza sehemu bandia za mwili kama vidole, masikio, pua, mikono, miguu, na kifua, ambazo zinaonekana kama kweli kwa watu wenye ngozi ya giza. Amanam pia hutoa huduma za bei rafiki na nafuu, wakati mwingine bure kwa watu wenye kipato kidogo kupitia mpango unaoitwa Ubokobong, unaomaanisha ‘Mkono wa Mungu’ katika lugha ya Ibibio

  1. AFRO, Special to the (2023-11-13). "Transforming lives with hyperrealism: The story of John Amanam, Nigerian prosthetic artist". Baltimore Afro-American (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2025-01-31.
  2. "John Amanam: The Nigerian Sculptor Who Creates Dark-Skin Prosthetics for Black Amputees". qazini.com (kwa Kiingereza). 2022-01-24. Iliwekwa mnamo 2025-12-14.
  3. "TEDxMaitama | TED". www.ted.com. Iliwekwa mnamo 2025-12-14.
  4. George, Godfrey (2021-05-22). "Accident which claimed my brother's fingers motivated me to start making prostheses – Sunday, Nigerian sculptor". The Punch (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2025-01-31.
  5. Bishara, Hakim (2021-02-09). "A Sculptor and Former Special Effects Artist Is Paving the Way in Prosthetics for Darker Skin Tones". Hyperallergic (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2025-01-31.
  6. "Transforming lives with hyper-realistic prostheses: The story of John Amanam, the first Nigerian prosthetic artist | NNPA". nnpa.org. Iliwekwa mnamo 2025-12-14.
  7. AFRO, Special to the (2023-11-13). "Transforming lives with hyperrealism: The story of John Amanam, Nigerian prosthetic artist". AFRO American Newspapers (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2025-12-13.
  8. George, Godfrey (2021-05-22). "Accident which claimed my brother's fingers motivated me to start making prostheses – Sunday, Nigerian sculptor". The Punch (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2025-01-31.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu John Amanam kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.