Johann Casimir Häffelin

Johann Casimir von Haeffelin (3 Februari 1737, Minfeld – 27 Agosti 1827, Roma) alikuwa kasisi wa Kanisa Katoliki katika dayosisi ya Speyer, kardinali, na mwanadiplomasia mashuhuri wakati wa utawala wa Maximilian I Joseph wa Bavaria.
Akiwa balozi wa Bavaria katika Makao Makuu ya Kanisa Katoliki, aliongoza mazungumzo ya Mkataba wa Concordat wa 24 Oktoba 1817 kati ya Ufalme wa Bavaria na Kanisa Katoliki chini ya Papa Pius VII. Mnamo 28 Septemba 1817, aliteuliwa kuwa askofu wa jimbojina la Chersonesus huko Krete na Papa Pius VII na akapewa daraja ya uaskofu tarehe 11 Novemba mwaka huo katika Kanisa la Maltheserkirche St. Michael huko Munich na Giulio Cesare Zoglio, balozi wa kitume.
Katika mkutano wa makardinali wa 6 Aprili 1818, Papa Pius VII alimteua kuwa kardinali, akipewa cheo cha Santa Sabina, ambacho baadaye mnamo 1822 kilibadilishwa kuwa Sant'Anastasia. Akiwa kardinali, alishiriki katika mkutano wa uchaguzi wa papa mwaka 1823, ambao ulimchagua Papa Leo XII.
| Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |