Nenda kwa yaliyomo

JoeyStarr

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
JoeyStarr
JoeyStarr mwaka 2012
Taarifa za awali
Jina la kuzaliwaDidier Morville
Amezaliwa27 Oktoba 1967 (1967-10-27) (umri 58)
Saint-Denis, Île-de-France, Ufaransa
Miaka ya kazi1988–sasa
Ameshirikiana naSuprême NTM, Kool Shen

Didier Morville (alizaliwa 27 Oktoba 1967), anajulikana zaidi kwa jina lake la kisanii JoeyStarr, ni rapa, mtayarishaji wa muziki na mwigizaji kutoka mjini Saint-Denis, Île-de-France, Ufaransa. Alianzisha kwa pamoja kundi la rap la Ufaransa Suprême NTM mwaka 1989 akiwa na Kool Shen.

Maisha na kazi

[hariri | hariri chanzo]

Utoto na malezi

[hariri | hariri chanzo]

JoeyStarr anatoka katika familia yenye asili ya Martinique, eneo la ng’ambo la Ufaransa. Alikulia katika mazingira magumu akiwa mtoto. Baba yake alikuwa mkali kupitiliza. Alipotimu umri wa miaka 18, alikutana na mama yake mzazi alitengana naye tangu akiwa na akiwa na umri wa miaka mitano. Miaka 18 baadaye walikutana.[1]

Mwaka 1985, alijiunga na jeshi katika mji wa Baden-Baden, uzoefu aliouelezea kama “miezi 19 ya mateso”, ambao pia ameutaja katika albamu Authentik.[2]

Baada ya kutoka jeshini, aliishi maisha ya mitaani, akilala kwenye vituo vya treni na vichochoroni. Ndipo alipogundua matumizi ya dawa za kulevya na utamaduni wa hip hop, ambao ulimbadilisha maisha.[3]

Suprême NTM

[hariri | hariri chanzo]
JoeyStarr (2007)

Wakati wa maisha ya mitaani, alikutana na rapa mwingine Kool Shen, ambaye pia alizaliwa Saint-Denis. Mwaka 1988 waliunda kundi la Suprême NTM.[4] Wimbo wao wa kwanza ulipotoka mwaka 1989, JoeyStarr hakuweza hata kuchukua malipo yake kwa sababu hakuwa na anwani wala akaunti ya benki.

Kundi hilo lilipata mafanikio makubwa kupitia albamu zao nne, kabla ya kuvunjika mwaka 1998. Lilirudi tena rasmi mwaka 2008.

Maisha binafsi

[hariri | hariri chanzo]

JoeyStarr alikutana na mwigizaji wa Ufaransa Béatrice Dalle mwaka 1994, na walikuwa katika uhusiano wa misukosuko kwa takriban miaka kumi.[5] Walitengana mwaka 2005 lakini waliendelea kuwa karibu kwa muda.

Ana watoto wawili, Mathis na Kalil, na mwandishi wa habari za hip hop Leïla Sy.

Mwaka 1999, alihukumiwa kifungo cha miezi miwili jela kwa kumshambulia mhudumu wa ndege.[6] Pia aliwahi kuhukumiwa kwa makosa mengine ya unyanyasaji, na rekodi yake ya makosa ina jumla ya makosa 13. Mwaka 2003 alikosolewa vikali baada ya kumdhuru mnyama kwenye televisheni ya taifa.

Tuzo na uteuzi

[hariri | hariri chanzo]
Muziki
  • 2007: Msanii bora wa rap (L'Année du hip-hop)
  • 2008: Tamasha bora la muziki
Uigizaji
  • 2010: Uteuzi wa mwigizaji bora wa nafasi ya pili (César Award)
  • 2012: Uteuzi mwingine wa César Award kwa filamu Polisse
  • 2012: Mshindi wa Tuzo ya Patrick Dewaere

Diskografia

[hariri | hariri chanzo]
  • La dernière année (2006)
  • Armageddon (2011)
  • Egomaniac (2011)
  • My Playlist (2006)
  • L'Anthology Mixtape (2007)

JoeyStarr ameigiza katika filamu nyingi, zikiwemo:

  • La Tour Montparnasse Infernale (2000)
  • Polisse (2011)
  • Alibi.com (2017)
  1. "JoeyStarr: la mauvaise réputation". Iliwekwa mnamo 2026-04-17.
  2. "Tous ces pédés de militaires..."
  3. "JoeyStarr: la mauvaise réputation". Iliwekwa mnamo 2026-04-17.
  4. Helenon, Veronique...
  5. "Béatrice Dalle révèle..."
  6. https://www.humanite.fr/... {{cite web}}: Missing or empty |title= (help)

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]