Joannah Stutchbury

Joannah Stutchbury (1954 - 2021) alikuwa mwanaharakati wa haki za ardhi na mazingira nchini Kenya. Alikuwa mmoja wa watetezi wakuu wa uhifadhi wa mazingira ya misitu ya Kenya, ambaye anakumbukwa kwa kujaribu kulinda msitu wa Kiambu dhidi ya uvamizi. Alisaidia Huduma ya Misitu ya Kenya. Alipigwa risasi na kuuawa tarehe 15 Julai 2021 [1][2][3] [4] akiwa na umri wa miaka 67. [5] Joannah alikuwa mpwa wa Jim Corbett . [6]
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Stutchbury alizaliwa karibu mwaka wa 1954 na aliishi Kiambu, ambao uko karibu kilomita ishirini kutoka katikati ya jiji la Nairobi. [7]
Alikuwa akiendesha kampeni dhidi ya waendelezaji wanaovamia Msitu wa Kiambu karibu na Nairobi. Asilimia 16 ya Kaunti ya Kiambu, ambayo ni hekta 40,000 imefunikwa na misitu. Miti hiyo hutumika kama kuni kwa sababu kuna mahitaji makubwa ya mkaa na kuni. Miradi ya upandaji miti inaendelea kwani miti inakabiliwa na joto linalozidi kuongezeka kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa. [8]
Stutchbury alikuwa ametangaza wazi upinzani wake dhidi ya wavamizi wa ardhi na waendelezaji binafsi waliotajwa. Mwaka wa 2018, aliingiya kwenye vichwa vya habari alipowakabili binafsi waendelezaji hao. Waendelezaji hao walikuwa wakikata miti katika Misitu ya Kiambu. Aliambiwa na watu wasiojulikana kwamba wangemuua ikiwa angeendelea kuingilia mpango wao wa kujenga barabara kupitia msitu huoi. [9]
Mnamo tarehe 15 Julai 2021, Joannah Stutchbury alipgwa risasi na kuuawa karibu na nyumba yake, ikisemekana ni kwa sababu ya kampeni yake dhidi ya uendelezaji ya maeneo wa ardhi oevu ndani ya mbuga ya kitaifa. Alisimamisha gari lake ili kuondoa matawi yaliyokua yameziba barabara ya kuingia nyumbani kwake ndipo aliposhambuliwa kwa kupigwa risasi mara kadhaa. Baadaye, majirani wake walipata mwili wake ndani ya gari. Injini ya gari bado ilikua ikiendelea kufanya kazi. Vitu vyake vya thamani vilikuwa bado ndani ya gari. Kutokana na kitendo hilo, ilihisiwa kuwa shambulio hilo halikuwa wizi. Stutchbury alikuwa amepaza sauti yake dhidi ya uvamizi na ujenzi wa miundombinu katika Msitu wa Kiambu uliokuwa karibu. Kabla ya tukio hilo, alikuwa amepokea vitisho vya kifo mara kadhaa, lakini aliendelea kusimama kidete kulinda mazingira hadi kifo chake. [10] [11] [12] Alikua na ardhi ambayo aliilinda kwa nguvu kwani alikataa kuiuza. alikua amezungumza kuhusu kuhamia kwingine kutokana na shinikizo alizokua akikumbana nazo. [13]
Hiki ilikua kifo cha kwanza cha mwanaharakati wa mazingira nchini Kenya kwa kipindi cha mwaka mmoja, ingawa wanaharakati wanane walikuwa wamefariki barani Afrika. [14] Hakukua na kukamatwa kwa haraka kwa waliohusika. [15] Shirika la dunia la Misitu (The World Forest Organisation) liliwasilisha ombi kwa rais wa Kenya, likimtaka alinda eneo la msitu huo katika ngazi ya kitaifa, kwa heshima ya Joannah. [16]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Joanna Stutchbury". Front Line Defenders (kwa Kiingereza). 2021-07-19. Iliwekwa mnamo 2022-04-26.
- ↑ "Who Was Joanna Stutchbury, Activist Shot Who Was Dead Following Threats" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-04-26.
- ↑ "Kenya: Concerns regarding the killing of Environmental Defender Joannah Stutchbury". UN SR Human Rights Defenders (kwa Kiingereza (Uingereza)). 2022-01-19. Iliwekwa mnamo 2022-04-26.
- ↑ "Kenya: Prominent environmental activist Joanna Stutchbury killed after receiving multiple death threats from developers". Business & Human Rights Resource Centre (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-11-27.
- ↑ "Environment activist shot dead outside Nairobi home after death threats". the Guardian (kwa Kiingereza). 2021-07-16. Iliwekwa mnamo 2024-11-27.
- ↑ "Jim Corbett's Great Niece And Environmentalist Joanna Stutchbury Shot Dead In Nairobi" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-11-27.
- ↑ Team, The (2021-07-16). "Another Murdered Environmentalist: Joannah Stutchbury – you'll be greatly missed". Word Forest (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2024-11-28.
- ↑ "Kiambu County attains 16pc forest cover – Kenya News Agency" (kwa Kiingereza (Uingereza)). 2022-05-22. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2024-11-11. Iliwekwa mnamo 2024-11-27.
- ↑ Pinnock, Don (2021-07-20). "OUR BURNING PLANET: Kenyan forest defender Joanna Stutchbury assassinated in gangster-style slaying". Daily Maverick (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-11-27.
- ↑ "Joanna Stutchbury". Business & Human Rights Resource Centre (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-11-27.
- ↑ "Kenya: Inquiétude de la société civile après le meurtre d'une célèbre écologiste qui luttait contre la déforestation causée par des promoteurs privés". Business & Human Rights Resource Centre (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-04-26.
- ↑ "Kenya: After almost two months, no arrests made for murder of conservationist threatened by road developers". Business & Human Rights Resource Centre (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-04-26.
- ↑ Panchal, Subodh (2021-08-08). "Joannah Stutchbury: She Lived for Her Forest". The America Times (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-11-27.
- ↑ Chege, Daniel. "227 environmentalists killed last year, new report shows as land activists push for State protection". The Standard (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-11-28.
- ↑ "Kenya: Prominent environmental activist killed after multiple death threats". Business & Human Rights Resource Centre (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-11-28.
- ↑ "Joannah Stutchbury Murdered for Protecting Kenya's Kiambu Forest | Permaculture magazine". 2022-03-08. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 8 Machi 2022. Iliwekwa mnamo 2024-11-27.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)