Nenda kwa yaliyomo

Jipu (rundu la usaha)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jipu (rundu la usaha)
Mwainisho na taarifa za nje
Kundi MaalumuUpasuaji wa jumla, Ugonjwa wa kuambukiza, magonjwa ya ngozi
DaliliWekundu, maumivu, uvimbe[1]
Muda wa kawaida wa kuanza kwakeKwa haraka
VisababishiMaambukizi ya bakteria (mara nyingi MRSA)[1]
Sababu za hatariMatumizi ya dawa kwa njia ya mishipa[2]
Njia ya kuitambua hali hiiUchunguzi wa mawimbi ya sauti (Ultrasound), Uchunguzi wa CT[1][3]
Utambuzi tofautiCellulitis, uvimbe wa sebaceous;, ugonjwa wa kuoza kwa nyama za mwili[3]
MatibabuChale na kutoa nje kiowevu[4]
Idadi ya utokeaji wake~1% kwa mwaka (Marekani)[5]

Jipu ni mlundikano wa usaha ndani ya tishu za mwili.[1] Ishara na dalili zake ni pamoja na wekundu, maumivu, joto na uvimbe.[1] Uvimbe huo unaweza kuhisiwa kujazwa na kiowevu wakati unapofinywa.[1] Eneo la wekundu mara nyingi ni kubwa zaidi ya uvimbe.[6] Majipu sugu (carbuncles) na majipu (boils) ni aina ya majipu ambayo mara nyingi huhusisha vinyeleo vya nywele, na majipu sugu yakiwa makubwa zaidi.[7]

Kwa kawaida, husababishwa na maambukizi ya bakteria.[8] Mara nyingi aina nyingi tofauti za bakteria zinahusika katika maambukizi moja.[6] Nchini Marekani na maeneo mengine mengi ya dunia, bakteria ya kawaida iliyopo ni Staphylococcus aureus inayostahimili methicillin.[1] Mara chache, vimelea (parasites) vinaweza kusababisha jipu; hii ni kawaida zaidi katika nchi zinazoendelea.[3] Utambuzi wake kawaida hufanywa kulingana na jinsi linavyoonekana na linathibitishwa kwa kulikata wazi.[1] Upigaji picha wa Ultrasound unaweza kuwa na manufaa katika hali ambazo utambuzi hauko wazi.[1] Katika majipu yaliyo karibu na njia ya haja kubwa, tomografia ya kompyuta (CT) inaweza kuwa muhimu katika kutafuta maambukizi ya kina zaidi.[3]

Matibabu ya kawaida ya majipu mengi ya ngozi au tishu laini ni kuzikata wazi na kutoa kiowevu kilicho ndani.[4] Inaonekana kuna faida fulani kutokana na kutumia pia antibiotiki; ingawa matumizi hayo yanahusishwa na madhara.[9][10] Ushahidi mdogo unaunga mkono kutopakia tundu ambayo inabakia kwa chachi baada ya kutoa kiowevu kilichokuwa ndani yake.[1] Kufunga tundu hili mara tu baada ya kutoa kiowevu kilichokuwa ndani yake badala ya kuliacha wazi kunaweza kuharakisha uponyaji bila kuongeza hatari ya jipu kurudi.[11] Kunyonya usaha kwa sindano mara nyingi haitoshi.[1]

Majipu ya ngozi ni ya kawaida tena yamekuwa ya kawaida zaidi katika miaka ya hivi karibuni.[1] Sababu za hatari ni pamoja na matumizi ya dawa kwa njia ya mishipa, na viwango vinavyoripotiwa kuwa vya juu kama 65% kati ya watumiaji.[2] Mnamo mwaka wa 2005 huko Marekani, watu milioni 3.2 walienda kwa idara ya dharura kwa sababu ya majipu.[5] Huko Australia, karibu watu 13,000 walilazwa hospitalini mnamo mwaka wa 2008 na hali hiyo.[12]

  1. 1.00 1.01 1.02 1.03 1.04 1.05 1.06 1.07 1.08 1.09 1.10 1.11 Singer AJ, Talan DA (Machi 2014). "Management of skin abscesses in the era of methicillin-resistant Staphylococcus aureus" (PDF). The New England Journal of Medicine. 370 (11): 1039–1047. doi:10.1056/NEJMra1212788. PMID 24620867. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2014-10-30. Iliwekwa mnamo 2014-09-24.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 Langrod, Pedro Ruiz, Eric C. Strain, John G. (2007). The substance abuse handbook. Philadelphia: Wolters Kluwer Health/Lippincott Williams & Wilkins. uk. 373. ISBN 9780781760454. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-09-06.{{cite book}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  3. 3.0 3.1 3.2 3.3 Marx, John A. Marx (2014). "Skin and Soft Tissue Infections". Rosen's emergency medicine : concepts and clinical practice (tol. la 8th). Philadelphia, PA: Elsevier/Saunders. ku. Chapter 137. ISBN 1455706051.
  4. 4.0 4.1 American College of Emergency Physicians, "Five Things Physicians and Patients Should Question", Choosing Wisely: an initiative of the ABIM Foundation, American College of Emergency Physicians, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Machi 7, 2014, iliwekwa mnamo Januari 24, 2014{{citation}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. 5.0 5.1 Taira, BR; Singer, AJ; Thode HC, Jr; Lee, CC (Machi 2009). "National epidemiology of cutaneous abscesses: 1996 to 2005". The American Journal of Emergency Medicine. 27 (3): 289–92. doi:10.1016/j.ajem.2008.02.027. PMID 19328372.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. 6.0 6.1 Elston, Dirk M. (2009). Infectious Diseases of the Skin. London: Manson Pub. uk. 12. ISBN 9781840765144. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-09-06.
  7. Marx, John A. Marx (2014). "Dermatologic Presentations". Rosen's emergency medicine : concepts and clinical practice (tol. la 8th). Philadelphia, PA: Elsevier/Saunders. ku. Chapter 120. ISBN 1455706051.
  8. Cox, Carol Turkington, Jeffrey S. Dover; medical illustrations, Birck (2007). The encyclopedia of skin and skin disorders (tol. la 3rd). New York, NY: Facts on File. uk. 1. ISBN 9780816075096. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-09-06.{{cite book}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  9. Vermandere, M; Aertgeerts, B; Agoritsas, T; Liu, C; Burgers, J; Merglen, A; Okwen, PM; Lytvyn, L; Chua, S (6 Februari 2018). "Antibiotics after incision and drainage for uncomplicated skin abscesses: a clinical practice guideline". BMJ (Clinical research ed.). 360: k243. doi:10.1136/bmj.k243. PMC 5799894. PMID 29437651.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  10. Ton, Joey (21 Januari 2019). "#227 There's Pus About, So Are Antibiotics In or Out? Adding antibiotics for abscess management". CFPCLearn. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 25 Machi 2023. Iliwekwa mnamo 16 Juni 2023.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  11. Singer, Adam J.; Thode, Henry C., Jr; Chale, Stuart; Taira, Breena R.; Lee, Christopher (Mei 2011). "Primary closure of cutaneous abscesses: a systematic review" (PDF). The American Journal of Emergency Medicine. 29 (4): 361–66. doi:10.1016/j.ajem.2009.10.004. PMID 20825801. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2015-07-22.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  12. Vaska, VL; Nimmo, GR; Jones, M; Grimwood, K; Paterson, DL (Jan 2012). "Increases in Australian cutaneous abscess hospitalisations: 1999-2008". European Journal of Clinical Microbiology & Infectious Diseases. 31 (1): 93–96. doi:10.1007/s10096-011-1281-3. PMID 21553298.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)