Jimbo Kuu la Juba
Mandhari
Jimbo Kuu la Juba (kwa Kilatini Archidioecesis Iubaensis) ni mojawapo kati ya majimbo 7 ya Kanisa Katoliki nchini Sudan Kusini na kama hayo yote linafuata mapokeo ya Kiroma.
Chini yake kuna kanda ya Kanisa yenye majimbo yafuatayo: Malakal, Rumbek, Tombura-Yambio, Torit, Wau na Yei.
Askofu mkuu wake ni Stephen Ameyu Martin Mulla.
Historia
[hariri | hariri chanzo]- 1927: Kuanzishwa kwa Apostolic Prefecture ya Bahr el-Gebel
- 1951: Kupandishwa cheo kuwa Apostolic Vicariate
- 1974: Kufanywa jimbo kuu
Uongozi
[hariri | hariri chanzo]Viongozi wote wa jimbo mpaka leo wamepatikana katika shirika la Wamisionari la mtakatifu Daniel Comboni.
Takwimu
[hariri | hariri chanzo]Eneo la jimbo lina kilometa mraba 25,137, ambapo kati ya wakazi 945,000 (2013) Wakatoliki ni 745,000 (sawa na 78.8%). Parokia ziko 12, mapadri ni 60 na watawa 76,
Hati rasmi za Papa kwa Kilatini
[hariri | hariri chanzo]- (Kilatini) Breve Expedit ut, AAS 19 (1927), p. 405
- (Kilatini) Bolla Si uberes fructus, AAS 43 (1951), p. 583
- (Kilatini) Bolla Cum in Sudania, AAS 67 (1975), p. 164