Jimbo Katoliki la Morogoro
Jimbo la Morogoro (kwa Kilatini: Dioecesis Morogoroensis) ni mojawapo katika ya majimbo 36 ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania kwa ajili ya waumini wake katika manispaa ya Morogoro pamoja na wilaya za Morogoro vijijini, Mvomero, Kilosa, Gairo n.k.
Eneo lote lina kilometa mraba 33,186.
Kutokana na historia yake linafuata mapokeo ya Kanisa la Kiroma, kama majimbo mengine yote ya Tanzania.
Makao makuu yako mjini Morogoro.
Kikanisa linahusiana na jimbo kuu la Dar-es-Salaam.
Historia yake
[hariri | hariri chanzo]- 11 Mei 1906: Kuundwa kama Apostolic Vicariate of Central Zanguebar kutokana na Apostolic Vicariate of Zanzibar
- 21 Desemba 1906: Kubadilishiwa jina kuwa Apostolic Vicariate of Bagamoyo
- 25 Machi 1953: Kupandishwa hadhi kuwa Diocese of Morogoro
- 7 Machi 2025: Kumegwa ili kuzaa Jimbo Katoliki la Bagamoyo
Uongozi wake
[hariri | hariri chanzo]- Vicars Apostolic of Bagamoyo
- Askofu François-Xavier Vogt, C.S.Sp. (1906.07.25 – 1923.05.19), kuhamishwa kuwa Vicar Apostolic of Cameroun
- Askofu Bartholomew Stanley Wilson, C.S.Sp. (1924.01.09 – 1933.05.23), kuhamishwa kuwa Vicar Apostolic of Sierra Leone
- Askofu Bernardo Gerardo Hilhorst, C.S.Sp. (1934.02.26 – 1953.03.25 tazama chini)
- Maaskofu wa Jimbo la Morogoro
- Askofu Bernardo Gerardo Hilhorst, C.S.Sp. (tazama juu 1953.03.25 – 1954.08.11)
- Askofu Herman Jan van Elswijk, C.S.Sp. (1954.07.18 – 1966.12.15)
- Askofu Adriani Mkoba (1966.12.15 – 1992.11.06)
- Askofu Telesphor Mkude (1993.04.05 – 2020.12.30) [1]
- Askofu Lazarus Vitalis Msimbe, S.D.S. (2019.02.13 – hadi sasa) kwanza kama Apostolic administrator sede plena[2] halafu sede vacante. Hatimaye alipewa daraja ya uaskofu tarehe 19-9-2021.
Papa analisimamia jimbo pia kupitia Idara ya Uinjilishaji wa Mataifa.
Kazi zake
[hariri | hariri chanzo]Likiishi katika eneo ambapo wananchi walio wengi ni Waislamu, linajadiliana nao kwa amani pamoja na kutangaza Injili ya Yesu Kristo.
Likitegemea uwezo wa Roho Mtakatifu katika liturujia linazidi kuwatakasa watu ili waishi kama watoto halisi wa Baba wa mbinguni.
Kwa mamlaka waliyokabidhiwa kwanza Mitume wa Yesu na kurithiwa kwa sakramenti ya daraja, linazidi kuwachunga waamini washuhudie upendo kati yao na kwa wote, hasa kwa kutumikia wanaohitaji huduma zake mbalimbali za kijamii pia (upande wa afya, elimu, n.k.).
Miundo na michango ya waamini mbalimbali
[hariri | hariri chanzo]Mbali ya ofisi na taasisi mbalimbali (k.mf. seminari), miundo yake ya msingi ni parokia zilizoenea katika wilaya zake zote na zinazoongozwa na mapadri wanajimbo na wanashirika, ambao baadhi yao ni wazawa, baadhi walitokea nchi za jirani na za mbali (hasa Asia na Ulaya).
Watawa wa kike na wa kiume wengi wa mashirika 40 hivi wanatoa mchango wa pekee kwa kushuhudia maisha ya Yesu katika useja mtakatifu, ufukara na utiifu.
Hatimaye walei, ambao ndio wanakanisa walio wengi, wanatimiza utume wao katika majukumu ya kila siku ya maisha ya kawaida vijijini na mitaani, wakishirikiana katika mtandao wa vigango, vinavyotegemea sana makatekista, na wa jumuia ndogondogo za Kikristo, zilizopewa kipaumbele na Sinodi ya Afrika.
Malengo
[hariri | hariri chanzo]Ni juhudi yao kulenga hali ya kujitegemea hata kiuchumi, ingawa hali halisi ya nchi ni ngumu kwa sababu zilezile zilizoathiri karibu nchi zote za bara hilo.
Wakitegemea neema ya Mungu, ni juhudi yao hasa kushinda dhambi ndani mwao wenyewe na ndani ya miundo ya jamii ili utawala wa Mungu uenee kote na kuleta utakatifu na wokovu, haki na amani.
Takwimu
[hariri | hariri chanzo]Baada ya kumegwa mwaka 2025 jimbo lilibaki na waamini waliobatizwa 680,435 kati ya wakazi 1,747,982 (38.9%).
Katika parokia 55 kulikuwa na mapadri 182 (wanajimbo 102 na watawa 80) na mabradha 7. Kabla ya kumegwa, kulikuwa na mafrateri watawa 444 na masista 691.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Kuanzia tarehe 13 Februari 2019 mamlaka yote jimboni imekabidhiwa na Papa Fransisko kwa Msimamizi wa Kitume padri Lazarus Vitalis Msimbe, SDS.
- ↑ "Rinunce e nomine, 13.02.2019". Vatican.va. Iliwekwa mnamo 13 Februari 2019.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- www.catholic-hierarchy.org katika ukurasa [1]
- Giga-Catholic katika ukurasa [2]
- [3] Ilihifadhiwa 11 Januari 2020 kwenye Wayback Machine. Tovuti rasmi ya jimbo
![]() |
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jimbo Katoliki la Morogoro kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |