Nenda kwa yaliyomo

Jessica Iskandar

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Jessica Iskandar (alizaliwa 29 Januari 1988) ni mwigizaji, mwanamitindo, mtangazaji, na mwimbaji wa Indonesia.[1] Pia anajulikana kwa jina la utani Jedar.

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Jessica Iskandar alizaliwa 29 Januari 1988 mjini Jakarta. Alikua katika familia yenye dini tofauti, ambapo baba yake Hardi Iskandar ni Muislamu na mama yake Wulandari ni Mkristo wa Kiprotestanti. Yeye ni mtoto wa mwisho wa familia na wa kike pekee akiwa na kaka wanne wakubwa.

Alimaliza elimu ya sekondari katika Bunda Mulia School. Kisha aliendelea na masomo katika Trisakti University, Jakarta, akichukua Interior Design. Baada ya mihula mitatu, aliacha chuo ili kuendelea na kazi yake ya sanaa.

Jessica Iskandar alianza kazi yake kama mwanamitindo baada ya kusoma katika John Casablanca modelling school. Alicheza filamu yake ya kwanza mwaka 2005 kama Kara katika filamu Dealova.[2] Filamu yake iliyofuata ilikuwa Diva (2007), iliyotengenezwa Malaysia.[3]

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jessica Iskandar kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  1. Bradley, Grant. "Stars get Indonesia hungry for NZ travel." New Zealand Herald. Saturday 17 November 2012. Retrieved 18 January 2013. "Indonesian celebrity chef Farah Quinn arrived yesterday to film cooking shows that will be fronted by model and actress Jessica Iskandar."
  2. "5 Transformasi Jessica Iskandar dari Perjuangannya di Film Dealova & Kini Siap Dipinang Richard Kyle". Tribunnews.com (kwa Kiindonesia). Iliwekwa mnamo 15 Julai 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "The Romantic Tale of Richard Kyle and Jessica Iskandar". Prestige Online – Taiwan (kwa American English). 14 Februari 2020. Iliwekwa mnamo 15 Julai 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)