Nenda kwa yaliyomo

Jesse Owens

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jesse Owens mwaka 1936.
Owens akiruka miruko mirefu katika mashindano ya Olimpiki.
Owens katika stempu ya Ajman (mmoja wa Falme za Kiarabu) mwaka 1971.

Jesse Owens (12 Septemba 191331 Machi 1980) alikuwa Mnegro (mtu mwenye asili ya Afrika) wa huko Marekani. Alipenda sana riadha na ndoto yake ilikuwa kuja kuwa mwanariadha mkubwa sana na maarufu pia.

Mwaka 1936 alikwenda kujisajiri katika mashindano ya kukimbia masafa marefu. Katika shindano lake la kwanza Jesse aliibuka mshindi. Aliendelea kushiriki katika mashindano mbalimbali, ndipo ikafikia hatua akapewa nafasi ya kwenda kushiriki katika mashindano ya Olimpiki huko Ujerumani, lakini familia yake haikupenda Jesse aondoke. Jesse akaamua kutoroka na kwenda kwenye mashindano. jambo lile liliisikitisha familia yake, ila baadaye wakakubali.

Alipowasili huko Ujerumani alipokewa kwa shangwe kubwa sana. Siku ya pili Jesse ilimbidi kuanza mashindano na alifanikiwa kushinda mashindano yote ndipo alichaguliwa kuingia fainali. Jesse alikuwa na furaha kubwa sana, siku ya fainali Jesse aliweza kushinda na kujinyakulia medali yake ya kwanza. halafu tatu kwa mkupuo mmoja.

Familia yake ilifurahi sana kwa mafanikio aliyopata mtoto wao, Jesse aliporudi kwao Marekani na medali nne. Alikuwa mwanariadha wa kwanza kupata medali nne kwa mkupuo mmoja na hii ilikuwa tukio la kihistoria.

Mnamo mwaka 1970 alipewa tuzo la ushujaa huko New York, kwa kuwa juhudi zake alizozifanya zilipelekea mafanikio yake kimichezo ambapo watu wengi sasa humfanya mfano wa kuigwa, bila kusahau heshima aliyoipa Marekani katika suala zima la michezo.

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jesse Owens kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.