Jean Gabin

Jean Gabin Alexis Moncorgé (alizaliwa Jean-Alexis Moncorgé, anajulikana kama Jean Gabin; 17 Mei 1904 – 15 Novemba 1976) alikuwa muigizaji na mwimbaji wa Ufaransa.[1] Akichukuliwa kama mtu muhimu katika tasnia ya filamu ya Ufaransa, aliigiza katika filamu kadhaa za kihistoria (classic films), zikiwemo Pépé le Moko (1937), La grande illusion (1937), Le Quai des brumes (1938), La bête humaine (1938), Le jour se lève (1939), na Le plaisir (1952).[2] Katika kazi yake, alishinda mara mbili tuzo ya Silver Bear kama Muigizaji Bora wa Kiume kutoka Tamasha la Kimataifa la Filamu la Berlin na tuzo ya Volpi Cup kama Muigizaji Bora wa Kiume kutoka Tamasha la Filamu la Venice. Gabin aliteuliwa kuwa mwanachama wa Légion d'honneur (nishani ya heshima ya juu kabisa nchini Ufaransa) kwa kutambua mchango mkubwa alioutoa katika tasnia ya filamu ya Ufaransa.[3]
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Gabin alizaliwa kama Jean-Alexis Moncorgé mjini Paris, akiwa mtoto wa kiume wa Madeleine Petit na Ferdinand Moncorgé, ambaye alikuwa mmiliki wa mgahawa na mtumbuizaji wa kumbi za starehe za usiku (cabaret) ambapo jina lake la jukwaani lilikuwa Gabin, ambalo ni jina la kwanza kwa lugha ya Kifaransa.[4]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ http://www.filmreference.com/Actors-and-Actresses-El-Ga/Gabin-Jean.html
- ↑ https://www.imdb.com/name/nm0300064/
- ↑ https://www.britannica.com/biography/Jean-Gabin
- ↑ https://www.fandango.com/people/jean-gabin-225773/biography
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jean Gabin kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
[Jamii:Waigizaji filamu wa Ufaransa]]