Jean-Clair Todibo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Todibo akiwa katika timu yake ya taifa.

Jean-Clair Dimitri Roger Todibo (amezaliwa 30 Desemba 1999) ni mchezaji wa soka wa Ufaransa ambaye anacheza kama beki wa kati au kiungo mkabaji wa Klabu ya FC Barcelona.

Todibo alianza kazi yake na klabu ya Toulouse mwaka 2016, kutoka FC Les Lilas. Alicheza mechi yake ya kwanza ya Ligue 1 mnamo 19 Agosti 2018 dhidi ya wapinzani wa Garonne Bordeaux, akicheza dakika 89 na kuibuka na ushindi wa 2-1 nyumbani.

Mnamo tarehe 8 Januari 2019, Todibo aliingia makubaliano na FC Barcelona wakati mkataba wake na Toulouse ulipokuwa umeisha. Alipewa jezi namba 6 mgongoni.


Football.svg Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jean-Clair Todibo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.