Nenda kwa yaliyomo

Janusz Marian Danecki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Janusz Marian Danecki, OFMConv (8 Septemba 195130 Agosti 2024) alikuwa askofu msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Campo Grande, Brazil, kutoka Polandi.

Danecki alijiunga na Shirika la Wadugu Wadogo Wakonventuali (Order of Friars Minor Conventual) mnamo 1971 akaweka nadhiri zake rasmi tarehe 8 Desemba 1975. Alipadrishwa tarehe 19 Juni 1977. Alitoa huduma ya upadre kwa miaka minane nchini Poland, akihudumu katika parokia mbalimbali pamoja na Jimbo Kuu la Warsaw hadi 1984.[1]

Mnamo tarehe 14 Aprili 1985, alitumwa kwenye Misheni ya Mtakatifu Maximilian Maria Kolbe nchini Brazil, iliyokuwa chini ya prelati ya Tefé.

  1. "Dom Mariano Danecki, bispo auxiliar de Campo Grande (MS), falece aos 73 anos - CNBB". www.cnbb.org.br (kwa Kireno (Brazili)). 30 Agosti 2024. Iliwekwa mnamo 31 Agosti 2024.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.