Janja
Mandhari
Janja | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
![]() Janja kungu (Lutjanus bohar)
| ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Spishi 73, 18 katika Afrika ya Mashariki:
|
Janja ni samaki wa baharini wa jenasi Lutjanus katika familia Lutjanidae ya oda Acanthuriformes katika ngeli Actinopterygii walio maarufu kwa matumizi. Majina mengine yatumikayo kwa spishi kadhaa ni tembo na kungu, lakini hayo hutumika pia kwa spishi za jenasi na familia nyingine. Wanatokea kwa kawaida katika maji ya kitropiki na kinusutropiki ya Bahari za Atlantiki, Hindi na Pasifiki kwenye miamba ya matumbawe na kapa. Spishi kadhaa wanatokea maji matamu au chumvi kidogo.
Jenasi hii ina spishi 73 duniani kote. Spishi 18 zimeriportiwa kutoka Afrika ya Mashariki.
Spishi za Afrika ya Mashariki
[hariri | hariri chanzo]- Lutjanus argentimaculatus, Chazanda (Mangrove red snapper)
- Lutjanus bengalensis, Janja wa Bengali (Bengal snapper)
- Lutjanus bohar, Janja Kungu (Twospot red snapper)
- Lutjanus ehrenbergii, Janja uso-kijivubuluu au tembo mbavaa (Blackspot snapper)
- Lutjanus fulviflamma, Janja madoa-meusi au kelea (Dory snapper)
- Lutjanus fulvus, Janja mkia-mweusi au tembo kaza (Blacktail snapper)
- Lutjanus gibbus, Haraki au numba (Humpback red snapper)
- Lutjanus johnii, Janja wa John (John's snapper)
- Lutjanus kasmira, Janja milia-buluu au tembo uzi (Common bluestripe snapper)
- Lutjanus lunulatus, Janja mkia-mwandamo (Lunartail snapper)
- Lutjanus lutjanus, Janja macho-makubwa au kitambue (Bigeye snapper)
- Lutjanus malabaricus, Janja wa Malabari (Malabar blood snapper)
- Lutjanus monostigma, Janja wa Shelisheli au changu kibaba (One-spot snapper)
- Lutjanus rivulatus, Janja chali (Blubberlip snapper)
- Lutjanus russellii, Janja wa Russell (Russell's snapper)
- Lutjanus sanguineus, Fuatundu au janja shogo (Humphead snapper)
- Lutjanus sebae, Dumbwara au janja mwekundu (Emperor red snapper)
- Lutjanus vitta, Janja milia-kahawia (Brownstripe red snapper)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Chazanda
-
Janja wa Bengali
-
Janja uso-kijivubuluu
-
Janja madoa-meusi
-
Janja mkia-mweusi
-
Haraki
-
Janja milia-buluu
-
Janja mkia-mwandamo
-
Janja macho-makubwa
-
Janja wa Malabari
-
Janja wa Shelisheli
-
Janja chali
-
Janja wa Russell
-
Fuatundu
-
Dumbwara
-
Janja milia-kahawia