Janga la Covid-19 Jiji la New York

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Janga la Covid-19 Jiji la New York: kesi ya kwanza inayohusiana na janga la COVID-19 ilithibitishwa huko Jiji la New York mwezi wa Machi mwaka 2020 kutoka kwa mwanamke aliyekuwa amewasili kutoka Iran, nchi ambayo ilikuwa tayari imekumbwa na janga hili. Baada ya mwezi mmoja eneo hili la mji mkubwa lilikuwa limeathirika zaidi nchini. Kufikia mwezi wa Aprili mji huu ulikuwa na kesi nyingi za coronavirus kuliko China, Uingereza, ama Irani, na kufikia mwezi Mei kulikuwa na kesi nyingi zaidi kuliko nchi nyingine yoyote isipokuwa Marekani penyewe.[1]

Mnamo Machi 20, ofisi ya gavana ilitoa agizo la watendaji kufungwa biashara zisizo za lazima. Mfumo wa usafirishaji wa umma jijini uliendelea kufanya kazi lakini ukawa na msongamano kwa sababu ya kupungua kwa huduma ya usafiri na ongezeko la watu wasio na makazi waliotafuta makazi kwenye mabehewa ya reli ya metro.[2]

Kufikia Aprili, mamia ya maelfu ya wakazi wa New York hawakuwa na kazi; serikali ya jiji ilipoteza mapato ya ushuru yanayo fikia mabilioni. Ajira za kipato cha chini katika sekta za rejareja, usafirishaji na mikahawa iliathiriwa haswa. Kushuka kwa mapato, ushuru wa mauzo na mapato ya utalii pamoja na mapato ya kodi ya hoteli iliweza kugharimu jiji hadi dola bilioni kumi. Meya Bill de Blasio amesema mfumo wa usaidizi kwa watu wasio na kazi wa jiji hilo ulianguka kufuatia kuongezeka kwa madai na zilihitaji msaada wa serikali kuu kudumisha huduma za kimsingi.[3]

Janga lilikuwa janga baya zaidi kwa idadi ya vifo katika historia ya jiji la New York.[4]

Baada ya kampeni ya kuchanja watu wengi katika miezi ya kwanza ya 2021, hali ilikuwa nafuu. Kwenye mwezi wa Mei huduma za usafiri wa metro zilirudishwa kwenye hali ya kawaida.

Picha[hariri | hariri chanzo]


Marejeo[hariri | hariri chanzo]