JamiiForums

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

JamiiForums ni tovuti ya mtandao wa kijamii iliyoko nchini Tanzania iliyoanzishwa mnamo mwaka 2006. Mtandao huo ni jukwaa maarufu mtandaoni. [1] [2]

Ukurasa wa kwanza wa JamboForum kabla ya kubadilika kuwa JamiiForums

JamiiForums ilizinduliwa rasmi mnamo Machi 2006 kwa jina la JamboForums, na ilikuwa na vikao kadhaa mkondoni. Mnamo Mei 2008 walibadilisha jina na kuwa JamiiForums kutokana na masuala ya hakimiliki. [3] Mnamo Machi 2016, Jamii Media iliwasilisha kesi dhidi ya jeshi la polisi la Shirikisho la Tanzania, ikidai matumizi ya nguvu ya jeshi la polisi kutaka habari za binafsi za watu wanaoshukiwa kuhusika na uhalifu ni kinyume cha katiba. Kesi hiyo itashughulikiwa kupitia Mahakama Kuu ya Tanzania. [4]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Science-symbol-2.svg Makala hii kuhusu mambo ya Mtandao wa Kijamii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu JamiiForums kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.