Nenda kwa yaliyomo

Jamie Uys

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Jacobus Johannes Uys (anajulikana zaidi kama Jamie Uys, 1921 - 1996) alikuwa mkurugenzi wa filamu wa Afrika Kusini, analijulikana zaidi kwa kuongoza filamu ya vichekesho ya mwaka 1980 The Gods Must Be Crazy pamoja na mwendelezo wake wa 1989 The Gods Must Be Crazy II. Uys pia aliongoza filamu ya kumbukumbu ya mwaka 1974 inayoitwa Animals Are Beautiful People.

Maisha ya Awali

[hariri | hariri chanzo]

Kabla ya kuingia katika tasnia ya filamu, Uys alikuwa mwalimu wa hisabati katika mji wake wa kuzaliwa wa Boksburg.[1]

Kisha alimuoa Hettie, ambaye pia alikuwa mwalimu wa hisabati, na wanandoa hao wakaanza kujishughulisha na kilimo pamoja na kufungua vituo vya biashara kando ya Mto Palala.

Baadaye aliteuliwa kuwa hakimu wa eneo husika na pia Hakimu wa Amani. Katika mahojiano, alisema, "Kila Jumanne nilivuka maeneo ya porini  kabisa na kuogelea kupitia mito ili kufika kituo cha polisi ambako ningeweza kuwasilisha kesi mahakamani".

Jamie Uys alifariki kutokana na mshtuko wa moyo mwaka 1996 akiwa na umri wa miaka 74 huko Johannesburg.[1]

  1. 1 2 Ap (1996-02-02), "Jamie Uys, 74, the Director Of 'The Gods Must Be Crazy'", The New York Times (kwa American English), ISSN 0362-4331, iliwekwa mnamo 2026-04-02