Jamie Carragher
Mandhari

James Lee Duncan Carragher (hutamkwa KARR-ə-ghər; alizaliwa 28 Januari 1978) ni mchambuzi wa soka kutoka Uingereza na mchezaji wa zamani aliyekuwa akicheza nafasi ya beki.
Akiwa mchezaji wa klabu moja pekee katika maisha yake ya soka, alikuwa makamu wa nahodha wa Liverpool kwa miaka kumi. Pia amefanya idadi ya pili kwa wingi ya mechi kwa klabu hiyo, huku akiwa mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi katika kipindi cha Ligi Kuu ya Uingereza (Premier League).
Carragher ni mshauri wa klabu ya Marine, inayoshiriki National League North.
Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]James Lee Duncan Carragher alizaliwa huko Bootle, tarehe 28 Januari 1978. Babu yake kwa upande wa mama alikuwa Mmalta, huku babu yake kwa upande wa baba akiwa Mwaireland.[1][2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://web.archive.org/web/20120623191347/http://www.liverpoolfc.com/team/first-team/player/jamie-carragher
- ↑ https://www.liverpoolfc.com/info/jamie-carragher
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jamie Carragher kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |