Jabir johnson
Makala hii inahusu mada au mtu asiyejulikana sana. Kuna mashaka kama mada inastahili kuwa na makala katika kamusi. Onyo hili linaweza kuwekwa pia kama makala haionyeshi umaarufu, hata kama upo.
Watumiaji wanaombwa kushiriki katika majadiliano kama makala hii inafaa kubaki au la. Tazama:Wikipedia:Umaarufu
Unaweza kuondoa kigezo hiki kama majadiliano yametokea na washiriki walipatana.
Jabir Johnson (Jabir J. Mking'imle) ni mwandishi wa habari na mtangazaji nchini Tanzania. Amekuwa maarufu kwa jina la Johnson Jabir. Alizaliwa mnamo tarehe 17 Agosti 1984 katika Hospitali ya Kibena, Njombe. Baba yake alifahamika kwa jina la Johnson Ananidze Mking'imle (1952-1998) na mama yake alifahamika kwa jina la Zera Adam Mahalamba (1956-2004). Ni miongoni mwa watoto wanane (8) wa Mzee Johnson Mking'imle. Kazi ya Uandishi wa Habari alianza mnamo mwaka 2007 akiwa mwaka wa pili katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Alianza kujitolea katika Redio moja jijini Dar es Salaam inayofahamika kwa jina la Praise Power Radio (Mwanzilishi wake ni marehemu Gertrude Rwakatare, mbunge wa zamani wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania). Amewahi kufanya katika Redio Mbeya FM, Baraka FM na Ushindi FM zote za mkoani Mbeya; Kili FM mkoani Kilimanjaro, Kiss FM jijini Dar es Salaam. Katika runinga amewahi kuwa ripota katika East Africa Television (EATV) kutoka Moshi. Katika magazeti amewahi kuandikia Mtanzania, Tanzania Daima na LaJiji kwa nyakati tofauti.[1]
- ↑ "Jabir Johnson". YouTube. Iliwekwa mnamo 2025-03-16.