Iyabo Obasanjo
| Iyabo Obasanjo | |
Obasanjo in 2015 | |
Senator for Ogun Central | |
| mtangulizi | Ibikunle Amosun |
|---|---|
| aliyemfuata | Olugbenga Onaolapo Obadara |
| tarehe ya kuzaliwa | 27 Aprili 1967 Lagos, Nigeria |
| chama | Peoples Democratic Party |
| ndoa | Oluwafolajimi Akeem Bello (m. 1999–2003) |
| watoto | 1 |
| mhitimu wa | |
| Fani yake |
|
Iyabo Obasanjo (alizaliwa Aprili 27, 1967) ni msomi mwanamke wa Nigeria, mtaalamu wa magonjwa ya mlipuko, na seneta wa huko nyuma nchini Nigeria. Yeye ni mtoto wa rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo na mke wa Oluremi Obasanjo .
Maisha ya awali na elimu
[hariri | hariri chanzo]Obasanjo alipata masomo yake Shule ya Corona kwenye eneo la Victoria Island, Lagos, Shule ya Capital maeeo ya Kaduna, na Chuo cha Queen eneo la Lagos. Alipata masomo ya shahada ya udaktari wa mifugo kutoka Chuo Kikuu cha Ibadan mwaka wa 1988, shahada ya uzamili juu ya epidemiolojia kutoka Chuo Kikuu cha California, Davis huko Davis, California, Marekani, mnamo 1990, na PhD katika somo hilo hilo kutoka Chuo Kikuu cha Cornell huko Ithaca, New York, mnamo 1994. [1]
Kazi ya kisiasa
[hariri | hariri chanzo]Enzi kabla hajachaguliwa kama seneta, Obasanjo alikuwa a afasi ya Kamishna wa Afya kwenye Jimbo la Ogun. [2] Aligombea tena kwenye uchaguzi wa Aprili 2011 kwenye jukwaa la PDP, lakini alishindwa na Olugbenga Onaolapo Obadara akapata ushindi wa kuongoza Bunge la Kitendo la Nigeria (ACN), kwa kuwa alipata kura 102,389 dhidi ya kura 56,312 za Obasanjo Bello. [3]
Kazi ya Seneti
[hariri | hariri chanzo]Obasanjo alichaguliwa kwenye Seneti mwaka 28 Aprili 2007 kwenye jukwaa la Chama cha Kidemokrasia cha Watu (PDP); mshindani mwenzake wa Action Congress (AC) Remilekun Bakare alikataa kabisa matokeo haya, japo Mahakama ya Maombi ya Uchaguzi ya Jimbo la Ogun ilitukuza ushindi wake.
Amewai kushika nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati ya Afya ya Seneti, na mjumbe mshirika wa Kamati za Usalama na Ujasusi, Usafiri wa Ardhini, Sayansi na Teknolojia, Elimu, Mipango ya Kitaifa, na Kamati za Bunge. [4] Alipoteza wadhifa wake kipindi cha Uchaguzi wa Bunge la Kitaifa mwaka 9 Aprili 2011.
Safari yake ya Utawala wake wa kisiasa hatimaye ulifikia kikomo mamo wa 2015 alipoangushwa na Seneta Gbenga Obadara ambaye alimnyang'anya wilaya ya Seneta ya Kati ya Ogun. [5]
Jaribio la mauaji
[hariri | hariri chanzo]Kwenye tarehe Aprili 2003, wakati wa siku ya uchaguzi mkuu gari lake lilifyatuliwa risasi kwenye Barabara ya Ifo ndani Jimbo la Ogun. Japo hakuwepo kwenye gari, watu wazima 3 na watoto 2 ndani ya gari walifariki. Wahalifu waliofanya hicho kitendo hawakuwahi kukamatwa. [6]
Uchunguzi wa EFCC
[hariri | hariri chanzo]Kwenye tarehe Aprili 2008, Obasanjo alifanyiwa uchunguzi na Tume ya Uhalifu wa Kiuchumi na Fedha ya Nigeria (EFCC) kutokana na uchunguzi uliomuungaisha na waziri wa zamani wa afya, Profesa Adenike Grange, na waziri wa afya wa nchi, Gabriel Aduku, kwa ubadhirifu wa fedha za umma. Wizara mwishoni mwa mwaka wa fedha haikurejesha pesa zote ambazo hazikutumika kwenye hazina ya serikali. Kiasi hicho kilikuwa Naira milioni 300, ambazo iasemekana ziligawanywa miongoni mwa waziri, waziri wake wa nchi na watumishi wakuu wa umma kwenye kamati ya afya ya Seneti na Baraza la Wawakilishi anayoisimamia. Waziri psmojs na naibu wake walilazimika kujiuzulu mara baada ya kurejesha sehemu yao ya pesa zile; hatimae walikamatwa na kuachiliwa kwa dhamana. Obasanjo aligoma kurejesha sehemu yake ya pesa hizo, naira milioni 10. Aliweka madai kwamba wanachama tisa wa kamati yake "walishawishi" fedha kutoka kwa wizara waliyoisimamia. Alitia mkazo kwamba pesa hizi zilitumika ndani ya mkutano kuhusu kuwajengea uwezo baadhi ya wanachama wa kamati ya afya waliohudhuria nchini Ghana. Mpaka sasa amekataa kujipeleka mbele ya EFCC. Japo aliitwa, kwa ujumla na waziri na watumishi wengine wa umma, alibisha kuwepo mahakamani. Wiki moja mbeleni, hali ya kutatanisha iliibuka wakati maafisa wa EFCC walipojaribu kumkamata nyumbani kwake ndani ya wilaya ya Maitama ya jiji la Abuja, baada ya kuwekewa dau kadhaa kwa wakati mmoja na maafisa wa utekelezaji wa sheria ambazo zilimsababisha kuruka juu ya uzio wake ili kuepuka kukamatwa na maafisa wa utekelezaji wa sheria wa Nigeria. Mwaka wa 2009 kesi hiyo ilitupiliwa mbali na Mahakama Kuu huko Abuja kwa madai kwamba haikuwa na mashiko yeyote. [7] [8]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Profile". Iyabo 4 Senate. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 19 Desemba 2007. Iliwekwa mnamo 22 Desemba 2007.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Aliteuliwa kama Seneta wa Nigeria mwenye kuwakilisha Wilaya ya Seneta ya Kati ya Ogun kwenye Jimbo la Ogun mwaka Aprili 2007. <ref name="nan">"Senator Iyabo Obasanjo-Bello". NAssNig.org. National Assembly of Nigeria. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 3 Machi 2016. Iliwekwa mnamo 21 Desemba 2007.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Obasanjo-Bello, Iyabo. "List of 2012 Fellows". Harvard University – Advanced Leadership Initiative. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 29 Mei 2013.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Senator Iyabo Obasanjo-Bello". NAssNig.org. National Assembly of Nigeria. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 3 Machi 2016. Iliwekwa mnamo 21 Desemba 2007.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)"Senator Iyabo Obasanjo-Bello". NAssNig.org. National Assembly of Nigeria. Archived from the original on 3 March 2016. Retrieved 21 December 2007. - ↑ "Iyabo Obasanjo". Harvard Advanced Leadership Initiative (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 25 Mei 2021. Iliwekwa mnamo 2021-05-22.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Four Die as Gunmen Shoot at Obasanjo's Daughter". Africa News Service. 23 Aprili 2003. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 4 Oktoba 2013.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Okon, Patrick Ene (2018). "Comparative Analysis of Mass Media Coverage of the Fight Against Corruption in Nigeria by the Obasanjo and Buhari Administrations". International Journal of Emerging Trends in Social Sciences. 4 (2): 47–57. doi:10.20448/2001.42.47.57.
- ↑ Owasanye, Bolaji (2014). Justice or Impunity: high profile corruption cases crawling or gone to sleep. Lagos: Human Development Initiatives. ISBN 9789789392506.