Nenda kwa yaliyomo

Iuliu Hossu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Iuliu Hossu
Kaburi la Hossu kwenye makaburi ya Bellu
Iuliu Hossu (kulia) akisoma katika Alba Iulia Azimio la Alba Iulia tarehe 1 Desemba 1918

Iuliu Hossu (30 Januari 188528 Mei 1970) alikuwa kiongozi wa Kanisa Katoliki la Kigiriki la Romania, aliyehudumu kama Askofu wa Cluj-Gherla.

Papa Paulo VI alimfanya Hossu kuwa kardinali kwa siri (in pectore) mwaka wa 1969, lakini uteuzi wake ulitangazwa baada ya kifo chake. Mamlaka ya Kikomunisti yalimkamata Hossu mnamo 28 Oktoba 1948. Kuanzia mwaka 1950 hadi 1955 alifungwa kama mfungwa wa kisiasa katika gereza la Sighet. Aliishi maisha yake yote akiwa chini ya kifungo cha nyumbani na alikufa mwaka 1970.

Anaheshimiwa katika Kanisa Katoliki kama mwenye heri mfiadini, baada ya kutangazwa na Papa Fransisko tarehe 2 Juni 2019.[1]

  1. "Servant of God Iuliu Hossu". Santi e Beati. Iliwekwa mnamo 7 Agosti 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.