Itifaki ya Nagoya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Itifaki ya Nagoya (kwa Kiingereza: Nagoya Protocol on Access to Genetic Resources and the Fair and Equitable Sharing of Benefits Arising from Their Utilization) ni makubaliano ya kimataifa yaliyoafikiwa tarehe 29 Oktoba 2010 huko Nagoya, Japani kwenye mkutano wa nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Bioanwai. [1]

Baada ya kuidhinishwa na nchi 50 na Umoja wa Ulaya mnamo 14 Julai 2014, ilianza kutumika siku 90 baadaye, kuanzia tarehe 12 Oktoba 2014. [2].[3]

Itifaki ya Nagoya inaunda mfumo wa sheria ya kimataifa wa ufikiaji kwa rasilimali za kijenetiki na ugawaji sawa wa faida kutokana na matumizi yake. Kwa msingi wa ridhaa ya pande zote, usawa unalengwa kupatikana kati ya masilahi tofauti za nchi zenye asili ya rasilimali za kijenetikia na nchi ambako rasilimali za kijenetikia hutumiwa. [4] Zaidi ya yote, uharamia wa kibiolojia unaoshutumiwa na nchi zinazoendelea unalengwa kuzuiwa kwa njia hii.

Mifano ya uharamia ya kibiolojia yaani matendo hasi yanayotakiwa kuzuiwa ni pamoja na utoaji wa hataza kwa madawa yanayotokana na mimea iliyotumiwa katika tiba ya kiutamaduni wa watu fulani ambako kampuni kutoka nchi nyingine inasafisha dawa lenyewe na kuitumia kibiashara bila kushirikisha wagunduzi wa kiasili.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. International Institute for Sustainable Development: Summary of the Tenth Conference of the Parties to the Convention on Biological Diversity: 18-29 October 2010 vom 1. November 2010 (PDF; 2,8 MB) Archived 4 Machi 2016 at the Wayback Machine.
  2. UNEP: Nagoya Protocol on genetic resources and associated traditional knowledge comes into effect today, Pressemitteilung vom 12. Oktober 2014.
  3. Prathapan, K. Divakaran; Pethiyagoda, Rohan; Bawa, Kamaljit S.; Raven, Peter H.; Rajan, Priyadarsanan Dharma (2018). "When the cure kills—CBD limits biodiversity research". Science. 360 (6396): 1405–1406. Bibcode:2018Sci...360.1405P. doi:10.1126/science.aat9844. PMID 29954970. S2CID 206667464. Retrieved 28 November 2018.
  4. Convention on Biological Diversity: A new era of living in harmony with Nature is born at the Nagoya Biodiversity Summit (PDF; 167 kB), Presseerklärung vom 29. Oktober 2010