Nenda kwa yaliyomo

Islam Slimani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Slimani akiwa na Algeria mwaka wa 2014

Islam Slimani (alizaliwa 18 Juni 1988) ni mchezaji wa kandanda kutoka Algeria anacheza nafasi ya kiungo mshambuliaji katika klabu ya Liga I CFR Cluj.

Slimani alianza kazi yake ya kandanda nchini Algeria akiwa na JSM Chéraga na CR Belouizdad. Mnamo mwaka 2013, alihamia Ulaya na kujiunga na Sporting CP, ambapo alicheza na kufunga mara kwa mara katika misimu mitatu, akisaidia timu yake kushinda kombe la Taça de Portugal mwaka 2015. Mnamo 2016, Slimani alisajiliwa na Leicester City kwa ada ya rekodi ya pauni milioni 28. Baada ya msimu mmoja na nusu, alikopeshwa mara kadhaa mfululizo katika klabu za Newcastle United, Fenerbahçe na Monaco.Mnamo 2021, Slimani alijiunga na Lyon, na mwaka mmoja baadaye alirudi Sporting CP na kudumu kipindi kifupi kwani aliondoka miezi sita baadae. Baada ya hapo alienda kujiunga na Brest, Anderlecht, Coritiba, na Mechelen kwa kipindi kifupi tena. Mnamo 2024, alirudi Algeria na kujiunga na CR Belouizdad, kisha kupelekwa kwa mkopo Westerlo mwaka 2025.[1]

Kama mchezaji wa kimataifa wa Algeria, Slimani alicheza debi yake mwaka 2012 na kucheza katika Africa Cup of Nations ya 2013, 2015, 2017, 2021, na 2023. Pia alikuwa sehemu ya kikosi cha Algeria kilichoshinda AFCON 2019. Alikuwa pia sehemu ya kikosi cha Algeria kwenye FIFA World Cup 2014, ambapo alimaliza kama kinara wa mabao wa timu pamoja na wenzake kwa kufunga mabao 2. Hadi Januari 2024, amecheza zaidi ya michezo 100 ya kimataifa na kufunga mabao 45, akiwa kinara wa mabao wa juu kabisa katika historia ya Algeria.[2]

  1. "Division 1 1e j MCO 4–1 CRB". DZFoot. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 3 Machi 2016. Iliwekwa mnamo 8 Januari 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Amical : l'Algérie s'impose difficilement contre le Bénin". L'Équipe (kwa Kifaransa). 9 Septemba 2019. Iliwekwa mnamo 9 Septemba 2019.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Islam Slimani kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.