Nenda kwa yaliyomo

Isco

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Isco akimiliki mpira dhidi ya Atletico Madrid

Fransisco Román Alarcón Suárez (maarufu kama Isco; alizaliwa 21 Aprili 1992) ni mchezaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Hispania anayecheza kama kiungo mshambuliaji. Ni mchezaji anayejulikana kuwa ni mmoja kati ya viungo washambuliaji bora kabisa duniani.

Alianza kucheza kwenye klabu ya Valencia kabla ya kuhamia Málaga mwaka 2011.

Kujituma kwake kulimwezesha kushinda tuzo ya mchezaji mdogo anayejituma Golden Boy mwaka 2012, na baadaye kununuliwa na Real Madrid mwezi Juni 2013 kwa ada ya £ milioni 30.

Isco alishinda mataji manne ya UEFA Champions League.

Pia ameisaidia nchi ya Hispania kwenye ngazi ya vijana kwenye Olimpiki mwaka 2012.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Isco kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.