Irv Gotti
| Irv Gotti | |
|---|---|
Gotti in 2005 | |
| Taarifa za awali | |
| Jina la kuzaliwa | Irving Domingo Lorenzo Jr. |
| Pia anajulikana kama |
|
| Amezaliwa | Juni 26, 1970 New York City, U.S. |
| Amekufa | 5 Februari 2025 (umri 54) |
| Kazi yake | Mtayarishaji wa rekodi, DJ, mtunzi wa nyimbo |
| Miaka ya kazi | 1985–2025 |
| Studio |
|
Irving Domingo Lorenzo Jr. (Juni 26, 1970 – Februari 5, 2025[1]) maarufu kwa jina lake la kisanii kama Irv Gotti au DJ Irv, alikuwa mtayarishaji wa rekodi za muziki kutoka nchini Marekani. Alianzisha lebo ya muziki Murder Inc. Records mwaka 1998, ambayo ilikuwa tawi la Def Jam Recordings. Gotti anahusishwa na kugundua au kusaini wasanii wa rap kama Jay-Z, DMX, na Ja Rule, pamoja na waimbaji Ashanti na Lloyd.[2][3]
Gotti alikuwa mtayarishaji mkuu wa albamu za kwanza za DMX (It's Dark and Hell Is Hot), Ja Rule (Venni Vetti Vecci), Ashanti (Ashanti), na Lloyd (Southside). Alipata sifa za utayarishaji kwa sehemu kubwa ya nyimbo zilizorekodiwa na wasanii waliokuwa wamejiunga na lebo yake—akiwemo Ja Rule (Rule 3:36, Pain Is Love, The Last Temptation, R.U.L.E.), The Inc. (Irv Gotti Presents: The Inc.), Ashanti (Chapter II, Concrete Rose), na Lloyd (Street Love)—pamoja na nyimbo za wasanii wengine kama Jennifer Lopez (I'm Real (Murder Remix), Ain't It Funny (Murder Remix)), Fat Joe (What's Luv), Eve (Gangsta Lovin'), na Kanye West (Violent Crimes) na wengine wengi.
Jarida la Rolling Stone[4] na gazeti la The New York Times yaliwahi kumtaja Gotti kama mmoja wa wabunifu wakuu wa mtindo wa mchanganyiko wa hip-hop na R&B mwishoni mwa miaka ya 1990 na mwanzoni mwa miaka ya 2000. Alipata vibao 28 vilivyoingia kwenye chati ya Billboard Hot 100, ambapo vinne vilifikia nafasi ya kwanza. Mwaka 2002, Gotti aliweka rekodi ya Guinness World Record kwa kutayarisha wimbo wa Billboard Hot 100 ulioshikilia nafasi ya kwanza kwa wiki kumi na tisa mfululizo. Alishinda tuzo ya Grammy mwaka 2003 na alipata uteuzi mwingine mwaka 2004, zote zikiwa kwa kazi yake na Ashanti. Pia alishinda tuzo 17 za BMI Awards, alitajwa kama BMI Songwriter of the Year miaka ya 2003 na 2004, na aliteuliwa mara mbili kwa tuzo za MOBO Awards mnamo 2002 na 2003.
Katika miaka ya mwisho ya 2000, Gotti alihamia kwenye televisheni na kuanza kuigiza kwenye kipindi cha uhalisia cha VH1, Gotti’s Way, kilichoonyeshwa kati ya 2007 na 2009. Alikuwa muanzilishi wa mfululizo wa BET Tales (2017–2022), ambacho kilitayarishwa kupitia kampuni yake ya uzalishaji wa burudani, Visionary Ideas. Mnamo Julai 2022, baada ya kuuza haki za rekodi zake za muziki kupitia makubaliano ya mamilioni ya dola na Iconoclast, Gotti alikuwa na miradi mingine ya filamu na vipindi vya televisheni hadi wakati wa kifo chake.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Irv Gotti, who created hits for Jennifer Lopez and Ja Rule, dies at 54". www.bbc.com (kwa Kiingereza (Uingereza)). 2025-02-06. Iliwekwa mnamo 2025-03-01.
- ↑ Rashbaum, William K.; Sweeney, Matthew (2005-12-03), "Hip-Hop Producers Get Acquittal, Then Hugs, From Jurors", The New York Times (kwa American English), ISSN 0362-4331, iliwekwa mnamo 2025-03-01
- ↑ Marc W. Dolech (2003-01-06). "Irv Gotti's Office Raided". Rolling Stone (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2025-03-01.
- ↑ Andre Gee (2025-02-10). "The Late Irv Gotti Personified the Highs and Lows of Genius". Rolling Stone (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2025-03-01.