Irene Kitchings
Irene Armstrong Wilson Kitchings (1908 hivi - 4 Machi 1975) alikuwa mpiga piano wa muziki wa jazz, kiongozi wa bendi, na mtunzi wa nyimbo mwenye na asili ya Afrika kutoka Marekani. Alitumbuiza kama msanii wa kujitegemea na pia akiwa na bendi mbalimbali. Kitchings alishiriki katika kuandika nyimbo "Some Other Spring", "Ghost of Yesterday", na "I'm Pulling Through", ambazo zote zilirekodiwa na Billie Holiday.
Maisha na kazi
[hariri | hariri chanzo]Irene Kitchings alizaliwa Violet Irene Armstrong huko Marietta, Ohio.[1][2] Mwaka wake wa kuzaliwa ni 1903 au 1908. Akiwa mtoto, aliishi Muncie, Indiana, pamoja na wazazi wake na dada yake, Grace. Alihamia Detroit akiwa na umri wa miaka 13 kuishi na shangazi. Mama yake alimfundisha kucheza piano akiwa mtoto.[2]
Akiwa na umri wa miaka 18, Kitchings alikuwa akiishi Chicago na akitumbuiza katika vilabu vya jazz kama mpiga piano wa jazz wakujitegemea na mwanachama wa bendi mbalimbali. Wakati mwingine alitumia jina la kisanii Irene Armstrong Edie. Bendi moja iliyoongozwa na Kitchings ilijumuisha wanamuziki kama Budd Johnson, Walter Fuller, na Dolly Jones.[2]
Kitchings alifunga ndoa na mpiga piano wa jazz anayeitwa Teddy Wilson karibu mwaka 1931. Wanandoa hao walihamia New York mnamo mwaka 1934, ambapo Wilson alijiunga na Benny Goodman Trio.[2] Kitchings aliacha kutumbuiza baada ya kuhamia New York.[3]
Kitchings alikutana na kuwa rafiki wa Billie Holiday baada ya wanawake hao wawili kutambulishwa na Wilson. Baada ya Kitchings kuachana na Wilson, Holiday alimtambulisha kwa mtunzi wa nyimbo na mtunzi, Arthur Herzog, Jr. Kwa pamoja, Herzog na Kitchings waliandika "Some Other Spring", wimbo ambao ulirekodiwa kwa mara ya kwanza na Holiday. Nyimbo zao mbili zingine ni "Ghost of Yesterday," na "I'm Pulling Through", ambazo pia zilirekodiwa na Holiday.
Kitchings, ambaye alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Eales, aliugua na kuhamia Cleveland kuishi na shangazi yake. Alipokuwa Cleveland, alikutana na kufunga ndoa na Elden Kitchings, akajifunza kupiga kinanda, na akawa mshiriki hai kanisani kwake.[1][2]
Kifo na urithi
[hariri | hariri chanzo]Kitchings alifariki mwaka 1975.[1]
Waandishi na wanahistoria mara nyingi humchanganya Kitchings na Irene Higgenbotham, ambaye ni mtunzi wa nyimbo na mpiga kinanda wa Kiafrika-Amerika, na ambaye pia aliandika nyimbo zilizowahi kuimbwa na Billie Holiday.[1]
Mwimbaji wa muziki wa Jazz Carmen McRae alimtambua Kitchings kama mlezi na mshauri. [4]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- 1 2 3 4 "A Tale of Two Irenes | WNYC | New York Public Radio, Podcasts, Live Streaming Radio, News". WNYC (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-03-26.
- 1 2 3 4 5 Placksin, Sally (1982). American Women in Jazz: 1900 To The Present : Their Words, Lives, and Music. New York: Seaview Books.
- ↑ Green, Laura Gayle. "Research Guides: Lesser-Known Composer of the Month: Brief Sketches: Irene Kitchings". guides.lib.fsu.edu (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-03-26.
- ↑ "Carmen McRae: 'Painter of Song'". NPR.org (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-03-26.