Nenda kwa yaliyomo

Ippolito d'Este

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ippolito (I) d'Este (kwa Kihungaria: Estei Hippolit; 20 Machi 14793 Septemba 1520) alikuwa kardinali wa Kanisa Katoliki kutoka Italia, na Askofu Mkuu wa Esztergom, Hungaria. Alikuwa mwanachama wa ukoo wa kikabaila wa Este ya Ferrara, na kwa kawaida alijulikana kama Kardinali wa Ferrara. Ingawa alikuwa askofu wa dayosisi tano tofauti, hakuwahi kuwekwa wakfu kuwa askofu. Alitumia muda wake mwingi kusaidia nyumba ya kidukali ya Ferrara na kujadiliana kwa niaba yao na Papa.[1][2][3]

  1. Lucy Byatt, Dizionario Biografico degli Italiani 43 (1993).
  2. Conradus Eubel, Hierarchia catholica medii aevi, sive Summorum pontificum, S.R.E. cardinalium, ecclesiarum antistitum series, editio altera, Tomus II (Monasterii 1913), p. 242.
  3. Sanuto gives the departure date as the 14th. Marino Sanudo (1879). F. Stefani (mhr.). I diarii di Marino Sanuto: (MCCCCXCVI-MDXXXIII) (kwa Kiitaliano). Juz. la Tomo I. Venezia: F. Visentini. uk. 44.
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.