Ion Iliescu

Ion Iliescu (3 Machi 1930 – 5 Agosti 2025) alikuwa mwanasiasa na mhandisi kutoka Romania ambaye alihudumu kama Rais wa kwanza na wa tatu wa Romania baada ya nchi hiyo kuingia kwenye mfumo wa demokrasia. Alishika wadhifa huo kuanzia mwaka 1989 hadi 1996, na tena kutoka mwaka 2000 hadi 2004. Iliescu alikuwa seneta kupitia Chama cha Kijamaa cha Demokrasia (PSD), ambacho alikianzisha na akabaki kuwa rais wa heshima wa chama hicho hadi mwisho wa maisha yake.
Iliescu alijiunga na Chama cha Kikomunisti cha Romania (PCR) mwaka 1953 na kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho mwaka 1965. Kuanzia mwaka 1971, Ceaușescu alianza kumweka kando kisiasa (Rais wa nchi hiyo). Alikuwa na nafasi ya uongozi katika Mapinduzi ya Romania, na akawa rais wa nchi hiyo mnamo Desemba 1989. Mnamo Mei 1990, alichaguliwa kuwa kiongozi wa kwanza wa taifa kwa njia huru ya kidemokrasia. Baada ya katiba mpya kupitishwa kupitia kura ya maoni, alihudumu kwa mihula miwili zaidi – kutoka 1992 hadi 1996, na baadaye kutoka 2000 hadi 2004 – mihula ambayo ilitenganishwa na Rais Emil Constantinescu, aliyemshinda katika uchaguzi wa 1996.[1][2][3]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Dosarul "Revoluției". Ion Iliescu este, oficial, urmărit penal pentru infracțiuni contra umanității" (kwa Kiromania). Știrile Pro TV. 17 Aprili 2018. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 18 Aprili 2018.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Dosarul Revoluției, în care Ion Iliescu e acuzat de infracțiuni împotriva umanității, a fost restituit de ÎCCJ la Parchetul Militar". www.digi24.ro (kwa Kiromania). Na. 22 June 2020. Iliwekwa mnamo 27 Agosti 2021.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Procesul împotriva lui Ion Iliescu, acuzat de „infracţiuni contra umanităţii" în Dosarul Revoluției, poate începe (Curtea de Apel)". www.digi24.ro (kwa Kiromania). 2023-10-25. Iliwekwa mnamo 2023-12-13.
| Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ion Iliescu kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |