Insha zisizo za kisanaa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Insha zisizo za kisanaa ni aina ya insha ambayo haitumii lugha za kifasihi isipokuwa hutumia lugha ya kawaida tu.

Katika insha hizo hakuna matumizi ya methali, nahau, vitendawili, misemo, tamathali za semi na kadhalika. Insha hizi kwa kawaida huwa na mada fulani anayoilenga mwandishi. Kwa mfano mwandishi anaweza kuwa ameambiwa aandike insha yenye mada 'umuhimu wa maji'

Muundo wa insha zisizo za kisanaa[hariri | hariri chanzo]

  • Madhumuni ya mwandishi
  • Utafiti
  • Kuongeza viungo vya nje

Madhumuni ya mwandishi[hariri | hariri chanzo]

Muundo wa insha zizizo za kisanaa huanza kwa madhumuni ya uandishi ule. Mwandishi anafaa aeleze hadhira yake kwa nini ameamua kuuandika mtungo ule, pia awaeleze ni mambo gani atakayoyaangazia katika mtungo wake ule.

Utafiti[hariri | hariri chanzo]

Mwandishi atafuatiliza madhumuni yake na utafiti alioufanya. Atawaeleza wasomaji ni yapi aliyokumbana nayo ili apate tamaa ya kuandika mtungo ule. Utafiti wake ndio utakaowafanya wasomaji waelewe ni kwa nini akaamua kuandika jinsi alivyoandika.

Kuongeza viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Katika insha za vyuo vikuu, wanafunzi yafaa waongeze viungo vya nje ambako walifanya utafiti wao. Kwa mfano, kama umepata takwimu kuhusu watu wasio na maji ulimwenguni kutoka kitabu fulani, yafaa unukuu hicho kitabu kama kiungo chako cha nje. Kwa kufanya hivi, msomaji ataweza kukibukua kitabu hicho ahakiki kama uliyosema yana ukweli.

Usiponukuu kule ulikofanya utafiti wako, basi itaonekana kuwa wewe ni mwizi uliyeiba kazi ya wengine. Wizi huo kwa Kiingereza huitwa "Plagiarism".

Katika kunukuu kazi, huenda ukatumia mfumo wa APA, Turabian au MLA kulingana na maagizo uliyopewa na mwalimu wako. Pia kozi unayofanya itakusaidia katika maamuzi hayo. Kwa mfano wanafunzi wanaofanya kozi za saikolojia au sosholojia hutumia APA, ilhali wanaofanya kozi za udaktari na uuguzi hutumia MLA.

Globe of letters.svg Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Insha zisizo za kisanaa kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.