Nenda kwa yaliyomo

Imbolo Mbue

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Imbolo Mbue
Amezaliwa1981
Kazi yakeMhandishi wa hadithi fupi na riwaya
TuzoPEN/Faulkner Award for Fiction na the Blue Metropolis Words to Change Award

Imbolo Mbue (alizaliwa Limbé, Kamerun, 1981) ni mwandishi wa riwaya na hadithi fupi mwenye asili ya Kamerun na uraia wa Marekani, anayeishi New York City.[1] Anajulikana kwa riwaya yake ya kwanza Behold the Dreamers (2016), ambayo ilimpatia Tuzo ya PEN/Faulkner kwa Riwaya Bora na Tuzo ya Blue Metropolis Words to Change.[2] Kazi zake zinatokana na uzoefu kutoka katika maisha yake kama mhamiaji pamoja na uzoefu wa wahamiaji wengine.

Maisha na elimu

[hariri | hariri chanzo]

Mbue alizaliwa katika eneo la nchi linalozungumza Kiingereza, ambako alikulia hadi pale familia yake ilipomfadhili kuendelea na masomo ya juu nchini Marekani.[3]

Baada ya kumaliza masomo yake ya shahada na ya uzamili, alianza kufanya kazi katika idara ya masoko ya kampuni ya vyombo vya habari, kazi ambayo aliipoteza wakati wa mdororo wa uchumi. Katika kipindi hicho, Mbue alitambua tofauti za kitabaka alipokuwa akitembea jijini New York, ambako aliona madereva wa teksi wengi wao wakiwa weusi wakisubiri kuwahudumia wakuu wa makampuni. Tukio hilo ndilo lililompa msukumo wa kuandika riwaya yake Behold the Dreamers (2016).[4]

  1. https://www.imbolombue.com/about/
  2. https://web.archive.org/web/20180731183549/http://www.penfaulkner.org/2017/04/04/announcing-the-2017-penfaulkner-award-winner/
  3. https://web.archive.org/web/20240713024501/https://www.oprah.com/oprahsbookclub/oprahs-book-club-imbolo-mbue-interview-august-2017-o-magazine
  4. https://www.rutgers.edu/news
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Imbolo Mbue kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.