Imane Abdelahad
Mandhari
Imane Abdelahad (kwa Kiarabu: إيمان عبد الأحد, alizaliwa tarehe 21 Julai 1994) ni mchezaji wa soka kutoka Morocco anayekipiga kama kipa kwa klabu ya SC Casablanca na timu ya taifa ya wanawake ya Morocco. Abdelahad alianza taaluma yake ya soka akiwa na umri wa miaka 15 katika klabu ya Wydad AC. Alishiriki msimu wa Ligi Kuu ya Wanawake ya Uturuki 2017–2018 akiwa na Beşiktaş J.K., ambapo alicheza mechi sita katika nusu ya pili ya msimu.[1] Baadaye alirejea Morocco na kucheza msimu mmoja na Ain Atiq na misimu miwili na Ittihad Tangiers kabla ya kujiunga na SC Casablanca. Tarehe 14 Novemba 2023, Abdelahad aliteuliwa kuwania tuzo ya Kipa Bora wa Mwaka 2023 na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).[2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Imane Abdelahad - Le football marocain au féminin". Youtube. 11 Februari 2020. Iliwekwa mnamo 13 Agosti 2023.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Morocco sweeps nominations in CAF awards for women's categories". HESPRESS English - Morocco News (kwa American English). 2023-11-14. Iliwekwa mnamo 2023-11-14.
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Imane Abdelahad kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |