Nenda kwa yaliyomo

Ildikó Rejtő

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ildikó Rejtő (anajulikana kama Györgyné Sági, awaliJenőné Újlaky; amezaliwa Budapest, Hungaria, 11 Mei 1937) ni mstaaafu wa Hungaria ambaye ni bingwa wa Olimpiki mara mbili na bingwa wa Dunia mara tano katika mchezo wa fencing (foil).[1][2]

Maisha yake ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa ni Myahudi.[3][4][5] Alizaliwa kiziwi.[6][7] Alikua na ugonjwa wa scoliosis tangu utotoni,[8] Hali hiyo ilimfanya baba yake kumsajili kwenye masomo ya fencing ili kusaidia kunyoosha mgongo wake.[9]

Kazi yake

[hariri | hariri chanzo]

Kwa sababu alikuwa kiziwi, alipoanza kucheza fencing akiwa na umri wa miaka 15, alijifunza kwa kusoma maelekezo yaliyoandikwa kutoka kwa makocha wake.[6][10]

Alishinda mashindano ya ulimwengu ya wasichana wa junior kwenye foil mwaka wa 1956–57, na alikuwa bingwa wa wanawake wa Hungary kwenye foil mwaka wa 1958.[11][12] Alikua mwanamichezo wa kike wa Hungary wa mwaka 1963 na mwaka 1964.[12]

Aliiwakilisha Hungary katika kila Michezo ya Olimpiki kuanzia mwaka 1960 hadi 1976 na alishinda medali saba za Olimpiki: dhahabu mbili (moja katika foil ya mtu binafsi na nyingine katika timu ya foil), fedha tatu (zote tatu katika timu ya foil), na shaba mbili (moja katika foil ya mtu binafsi na nyingine katika timu ya foil). Katika Michezo ya Olimpiki ya 1960 huko Roma akiwa na umri wa miaka 23, alishinda medali ya fedha ya timu katika foil ya wanawake.[13]

  1. Ildikó Rejtő-Ujlaky-Sági Archived 23 Julai 2016 at the Wayback Machine. sports-reference.com
  2. New Guinness Book of Records - Norris McWhirter, Ross McWhirter
  3. Taylor, P. (2004). Jews and the Olympic Games: The Clash Between Sport and Politics: with a Complete Review of Jewish Olympic Medalists. Sussex Academic Press. uk. 240. ISBN 9781903900888. Iliwekwa mnamo 20 Juni 2015.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Encyclopaedia Judaica - Fred Skolnik, Michael Berenbaum
  5. Encyclopedia of Jews in Sports
  6. 6.0 6.1 The Armchair Olympian: How Much Do You Know About Sport's Biggest Competition?
  7. Day by Day in Jewish Sports History - Bob Wechsler
  8. Rejtő Ildikó és Wichmann Tamás volt a Gépész vendége Archived 13 Agosti 2021 at the Wayback Machine. Sonline
  9. Előbb kisebbségi érzését, majd a világot mosta le. Index.hu
  10. The Incredible Fencer Ujlaky-Rejto Ildiko: The Deaf Olympic Champion – The Olympians
  11. "Uslaky-Rejto, Ildiko": Jews In Sports
  12. 12.0 12.1 "Seattle’s Derrick Coleman: another great deaf sportsperson"
  13. Ildikó Rejtő-Ujlaky-Sági | Olympics at Sports-Reference.com