Ikutaro Kakehashi
Ikutaro Kakehashi (Kijapani: 梯 郁太郎; 7 Februari 1930 – 1 Aprili 2017), anayejulikana pia kwa jina la utani Taro, alikuwa mhandisi, mvumbuzi na mjasiriamali wa Kijapani. Alianzisha kampuni za utengenezaji wa vyombo vya muziki za Ace Tone Roland Corporation na Boss Corporation, pamoja na kampuni ya vifaa vya sauti na picha ya ATV Corporation.
Kakehashi alianzisha Ace Tone mwaka 1960 kwa ajili ya kutengeneza ogani ya kielektroniki na mashine za awali za midundo (drum machine). Mwaka 1972 alianzisha Roland na kushiriki katika maendeleo ya vyombo mbalimbali vya muziki vya kielektroniki vilivyokuwa na ushawishi mkubwa, kama vile mashine za midundo za TR-808 na TR-909, pamoja na vinanda vya TB-303 na Juno-60. Pia alihusika katika maendeleo ya vifaa vya Boss kama vile vikuza sauti vya gitaa na pedali za athari za sauti.
Kakehashi alikuwa mmoja wa watu muhimu katika maendeleo ya MIDI, kiwango cha kiufundi kinachowezesha vyombo mbalimbali vya muziki vya kielektroniki kuunganishwa pamoja, katika miaka ya 1980. Mwaka 2013 alipokea Technical Grammy Award, akishirikiana na Dave Smith wa Sequential, kwa mchango wao katika uvumbuzi wa MIDI.[1]
Uvumbuzi wa Kakehashi umepewa sifa kubwa kwa kuathiri maendeleo ya aina mbalimbali za muziki maarufu duniani, zikiwemo muziki wa kielektroniki, muziki wa dansi, hip hop, R&B, muziki wa rock na muziki wa pop.[2][3]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ McKee, Ruth; Grierson, Jamie (2 Aprili 2017). ["Roland) founder and music pioneer Ikutaro Kakehashi dies aged 87". The Guardian.
{{cite news}}: Check|url=value (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ [(http://www.factmag.com/2017/04/02/ikutaro-kakehashi-life/) The life and times of Ikutaro Kakehashi, the Roland pioneer modern music owes everything to], Fact
- ↑ Pareles, Jon (3 Aprili 2017). ["Ikutaro) Kakehashi, Engineer Behind Revolutionary Drum Machine, Dies at 87". The New York Times.
{{cite news}}: Check|url=value (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ikutaro Kakehashi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |