Nenda kwa yaliyomo

Ikhtilaf

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Makala hii ni sehemu ya shindano la kuandika makala za Uislamu kupitia Wiki Loves Ramadan 2025.

Sehemu ya mfululizo wa makala juu ya

Uislamu

Imani na ibada zake

Umoja wa Mungu
Manabii
Misahafu
Malaika
Uteule
Kiyama
Nguzo za Kiislamu
ShahadaSwalahSaumu
HijaZaka

Waislamu muhimu

Muhammad

Abu BakrAli
Ukoo wa Muhammad
Maswahaba wa Muhammad
Mitume na Manabii katika Uislamu

Maandiko na Sheria

AzifQur'anSunnahHadithi
Wasifu wa Muhammad
Sharia
Elimu ya Sheria za KiislamuKalam

Historia ya Uislamu

Historia
SunniShi'aKharijiyaRashidunUkhalifaMaimamu

Tamaduni za Kiislamu

ShuleMadrasa
TauhidiFalsafaMaadili
Sayansi
SanaaUjenziMiji
KalendaSikukuu
Wanawake
ViongoziSiasa
Uchumi
UmmaItikadi mpyaSufii

Tazama pia

Uislamu na dini nyingine
Hofu ya Uislamu

Ikhtilāf (kwa Kiarabu:اختلاف; hutafsiriwa kama mgongano, tofauti) ni tofauti ya maoni ya kielimu ya kidini katika Uislamu, na hivyo ni kinyume cha ijma (makubaliano ya pamoja ya wanazuoni wa Kiislamu).

Mwongozo katika Qurani

[hariri | hariri chanzo]

Kulingana na Aya ya Utii, tofauti yoyote ya kidini inapaswa kutatuliwa kwa kurejea kwenye Qurani na Sunnah ili kuondoa ikhtilāf na kuepuka taqlid.[1][2] Ingawa wale wenye mamlaka hawakutajwa moja kwa moja katika aya hiyo, wanatajwa katika aya ya 4:83, inayoeleza: "Na wanapowafikia habari za amani au khofu, huieneza. Lakini wangelipeleka kwa Mtume na kwa wale wenye mamlaka miongoni mwao, bila shaka wale waliokuwa na uwezo wa kuielewa wangeliijua."[3] Hoja hii pia imehusishwa na Muhammad al-Baqir (114/732),[4] na inapatikana katika al-Jami' li-ahkam al-Quran ya msunni al-Qurtubi ( 671/1272).[3]

Hadith ya Mtume Muhammad isemayo kuwa "Allah hataruhusu ummah wangu wote wakakubaliana juu ya upotofu"[5] imetajwa katika vitabu vya Tirmidhi, Ibn Majah, Musnad Ahmad, na Darimi. Hadith hii mara nyingi hutumika kama hoja ya msingi ya Ijma na pia kupinga ikhtilaf kwa mtazamo wa Kisunni.

Baadhi ya wanazuoni wa Kiislamu hufundisha kuwa pale ambapo kuna tofauti ya maoni ya kielimu kuhusu jambo fulani, si halali kumhukumu mtu anayefuata maoni tofauti na ya mtu mwingine. Amri ya kuamrisha mema na kukataza maovu haifai kutekelezwa wakati kuna ikhtilaf juu ya msimamo.

Hata hivyo, kuna mashaka kuhusu usahihi wa tamko hili ikiwa kweli lilitoka kwa Mtume Muhammad au la. Watu hulitaja tamko hili kama hadith, lakini halipo kwenye vitabu sita vya hadith sahihi na mlolongo wa wapokezi wake haujulikani vizuri. Kuna matoleo mbalimbali ya tamko hili. Katika baadhi yake, inasemwa: "Tofauti ya maoni kati ya Maswahaba wangu ni rehema kwenu"; au "Tofauti ya maoni ya Maswahaba wangu ni rehema kwa Ummah wangu." Wanazuoni wengi wa hadith huliona tamko hili kuwa dhaifu au da'if kwa upande wa usimulizi wake.[6]

Neno ikhtilāf al-fuqahā au ikhtilāf al-fiqh, likiwa na maana ya "tofauti za wanazuoni wa fiqhi", linarejelea tofauti za maoni miongoni mwa wanazuoni wa fiqhi wa Kiislamu wa mwanzo na hasa aina ya maandiko yanayokusanya na kulinganisha maoni tofauti ya kifiqhi. Mikusanyo hii mara nyingi hupangwa kwa kufuata mada na hulinganisha mashule ya fiqhi au tofauti ndani ya shule fulani. Ikhtilāf al-fuqahā pia ni jina la kitabu kilichoandikwa na al-Ṭabarī.[7]

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Ad-Dahlawi, Waliyullah; Achmad, Bahrudin (19 Mei 2022). HISTORIOGRAFI IKHTILAF DALAM ISLAM: Al-Inshof fi Bayani Asbabil Ikhtilaf (kwa Kiindonesia). Almuqsith Pustaka. ku. 176–178. Iliwekwa mnamo 3 Desemba 2022.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Syirazi, Dr Abdul Karim Biazar (1 Januari 2015). Menuju Persatuan Islam: Pandangan Ulama Internasional (kwa Kiindonesia). Nur alhuda. uk. 110. ISBN 978-602-306-015-3. Iliwekwa mnamo 3 Desemba 2022.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. 3.0 3.1 Nasr et al. 2015, p. 533.
  4. Lalani 2000, pp. 63–4.
  5. Imepokelewa na al-Tirmidhi (4:2167), Ibn Majah (2:1303), Abu Dawood, na wengine kwa lafudhi tofauti kidogo.
  6. al-Suyuti al-Jami al-Saghir Ibn al-Hajib Mukhtasar
  7. John L. Esposito (ed.), The Oxford Dictionary of Islam (Oxford University Press, 2003), s.v. "Ikhtilaf al-Fiqh".

Vitabu vilivyonukuliwa

[hariri | hariri chanzo]