Idris al-Wathiq
Idris al-Wathiq (alifariki mwaka 1269), anayejulikana pia kama Abu Dabbus, alikuwa khalifa wa mwisho wa Waalmohadi aliye tawala mjini Marrakesh kuanzia mwaka 1266 hadi kifo chake.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Marrakesh ilikuwa imezingirwa hapo awali na sultani wa Wamarinidi Abu Yusuf Yaqub ibn Abd Al-Haqq kabla ya mwaka 1266, ingawa bila mafanikio. Idris alitumia fursa ya machafuko hayo kumwondoa binamu yake Abu Hafs Umar al-Murtada kwa msaada wa Abu Yusuf, na kujitangaza kuwa khalifa wa Waalmohadi, ingawa mamlaka yake yalikuwa ndani ya jiji pekee. Hata hivyo, mtawala wa Wamarinidi alibadili nia baadaye, na kumshawishi mtawala wa Wazayyanidi Yaghmurasen Ibn Zyan kushambulia Marrakesh. Mzingiro huo uliendelea kutoka mwaka 1268 hadi Septemba 1269, wakati jiji hilo lilipoanguka. Idris al-Wathiq alikamatwa na majeshi ya pamoja ya Wamarinidi na Wazayyanidi na kuuawa.
Kifo cha Idris kilihitimisha enzi ya Dola ya Waalmohadi.[1]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Julien, Charles-André. Histoire de l'Afrique du Nord, des origines à 1830, Payot, Paris, 1994.
| Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Idris al-Wathiq kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |