Ibrahim Musa
Ibrahim Musa (alifariki 7 Agosti 2025) alikuwa mwanasheria kutoka Nigeria aliyechaguliwa kuwa Seneta wa jimbo la Niger Kaskazini, mkoani Niger, Nigeria, katika uchaguzi wa kitaifa uliofanyika Aprili 2011.[1][2][3][4][5]
Historia ya Maisha
[hariri | hariri chanzo]Musa alitumia miaka 17 akifanya kazi kama mwanasheria. Wakati wa kufanya kazi hiyo, alikuwa mwanachama wa chama cha All Nigeria Peoples Party (ANPP). Baada chama cha Congress for Progressive Change (CPC) kuanzishwa, Musa aliamua kuwania kiti cha seneti kwa tiketi ya CPC.
Musa alifariki dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi tarehe 7 Agosti 2025.
Kazi ya Seneti
[hariri | hariri chanzo]Kupitia tiketi ya CPC, Musa alipata kura 131,872, akimshinda mpinzani wake aliyekuwa Seneta, Nuhu Aliyu wa chama cha People's Democratic Party (PDP), aliyepata kura 83,778.
Baada ya uchaguzi, Nuhu Aliyu, ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama ya Seneti, alikata rufaa kwenye tume ya rufaa za uchaguzi ya mkoa wa Niger dhidi ya Ibrahim Musa.
Musa alikamatwa Julai 2011 kwa tuhuma za kuwasilisha nyaraka za uongo kwenye Tume ya Rufaa za Uchaguzi huko Minna na alizuiliwa kwa siku nne. Septemba 2011, baada ya kuachiwa huru, Musa alisema kuwa wakati aliotumia akiwa gerezani ulimfanya awe na nguvu zaidi.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Ismail, Nana (7 Agosti 2025). "Former Niger North senator Ibrahim Musa dies". Daily Post. Iliwekwa mnamo 7 Agosti 2025.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Full election results from Niger State". Next (Nigeria). Aprili 12, 2011. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Agosti 15, 2011. Iliwekwa mnamo Juni 17, 2011.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Niger State Elections Petition tribunal Receives 21 Petitions". Channels TV. Mei 23, 2011. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Septemba 29, 2011. Iliwekwa mnamo Juni 17, 2011.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Folasade-Koyi, Adetutu (Juni 7, 2012). "One North is a thing of the past -Senator Musa". The Sun. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Machi 4, 2016. Iliwekwa mnamo Mei 3, 2013.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Hamagam, Aliyu (Julai 14, 2011). "Nigeria: CPC Condemns Arrest of Senator Ibrahim Musa". AllAfrica. Iliwekwa mnamo Januari 11, 2020.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
| Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ibrahim Musa kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |