Ibrahim Ajibu Migomba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Ibrahim Ajibu Migomba (alizaliwa katika mkoa wa Singida tarehe 12 Septemba 1996) ni mchezaji wa mpira wa miguu nchini Tanzania.

Uwanjani anatumia zaidi mguu wa kulia ingawa anaweza pia kucheza kama winga wa kushoto lakini kiasili Ajibu ni mshambuliaji wa kati.

Baada ya kulelewa na mzazi mmoja, mama yake pekee, wakahama Singida kuelekea Dar es Salaam ambako ndiko alikoanzia maisha ya soka huku akishindwa kupata elimu ya sekondari.

Ajibu alijiunga kwenye accademy ya klabu ya Simba mwaka 2009 akiwa na umri wa miaka 13 na aliichezea Simba under-20 kabla ya kupandishwa kwenye timu ya wakubwa mwaka 2013 akiwa na miaka 17.

Aliishi Simba kwa misimu 4 na kuondoka akaenda kujiunga na club ya Yanga Sc kwa mkataba wa miaka 2 ambao utamweka pale hadi katikati ya mwaka 2019. Huko Yanga katika mechi 55 alifunga magoli 46.

Ajibu ni mtaalamu wa pasi za mwisho (assist) ambapo katika ligi ya Tanzania 2018/19 ameweza kutengeneza magoli kumi (10) na akifunga 4 yeye mwenyewe.

Hadi sasa goli la Ajibu dhidi ya Mbao Fc linashika nafasi ya kwanza.

Ibrahim Ajib,baada ya kumaliza mkataba wake katika klabu ya Yanga kwa sasa amejiunga na klabu ya Simba sc kwa mkataba wa miaka miwili.

Ni muumini wa dini ya Kiislamu, ana mke na mtoto 1 wa kike. Pia ni mtaalamu wa kuogelea.

Football.svg Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ibrahim Ajibu Migomba kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.